Wavulana hupewa 13% pesa zaidi ya wasichana

Image caption Wavulana hupewa 13% pesa zaidi ya wasichana

Wazazi waliwapatia watoto wao wa kiume asilimia kumi na tatu ya pesa za matumizi kila wiki katika kipindi cha mwaka mmoja, huku pengo la kijinsia likipanuka kwa 2% mwaka uliotangulia, Utafiti umebaini

Utafiti huo wa kila mwaka kuhusu pesa za matumizi unaoendeshwa na kampuni ya Halifax, ulijumuisha zaidi ya watoto 1,200 na wazazi 575.

Aidha utafiti huu ulibaini kuwa watoto wa kiume wenye umri kati ya miaka minane na kumi na tano walipewa £6.93 kwa wiki ilihali watoto wa kike wakipewa £6.16 hiyo ikiashiria asilimia 6% ya wastani.

Haki miliki ya picha thinkstock
Image caption Watoto katika mji wa London wanapokea kiwango cha juu zaidi cha pesa za matumizi ikilinganishwa na wenzao katika eneo la mashariki la Anglia

Hii inamaanisha watoto wa kiume na kike wameshuhudia pesa zao za matumizi zikifikia kiwango kilichokisiwa mwaka 2007.

Halifax pia kupitia utafiti huo ilisema kulikuwa na baadhi wa watoto waliojumuishwa katika utafiti huo ambao wamekuwa wakipokea pesa kidogo za matumizi ya kibinafsi kutoka kwa wazazi wao kama ilivyo ada kwa kiwango cha kati ya asilimia 78% hadi 81%.

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Utafiti ulifichua kuwa asilimi 40% ya wavulana hawakuridhishwa na kiwango hicho cha pesa

Cha kushangaza pengine ni kuwa utafiti huo ulifichua kutoridhishwa kwa watoto hao na pesa za matumizi wanazopewa huku asilimia 40% kati yao wakipendekezwa wapewe pesa zaidi.

Halifax imekuwa ikiendesha utafiti kuhusu pesa za matumizi ambazo wazazi huwapatia watoto tangu mwaka wa 1987 alisema Giles Martin, ambaye ni mkuu wa kitengo cha kuweka akiba cha kampuni hiyo.

Watoto katika mji wa London wanapokea kiwango cha juu zaidi cha pesa za matumizi ikilinganishwa na wenzao katika eneo la mashariki la Anglia.