Watatu wauawa mechi ya amani Sudan Kusini

Sudan Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi kutoka Sudan wamekuwa wakigombana na wenyeji Sudan Kusini

Watu watatu wameuawa baada ya mapigano kuzuka wakati wa mechi ya soka iliyoandaliwa kuhimiza amani nchini Sudan Kusini.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi limesema limesema mkimbizi mmoja kutoka Sudan na raia wawili wa Sudan Kusini walifariki wakati wa mechi hiyo iliyokuwa ikichezewa eneo la Maban.

Eneo la Maban linapatikana kaskazini magharibi mwa Sudan Kusini, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Sudan.

Uhasama umekuwa ukiongezeka baina ya wakimbizi na wenyeji kwa wiki kadha, sana kuhusu wizi wa nguruwe na mbuzi.

Umoja wa Mataifa unasema vifo hivyo vimechochea makabiliano zaidi.

Watu wengi wameumizwa na nyumba kadha kuchomwa.

Sudan Kusini ilijipatia uhuru wake baada ya kujitenga kutoka kwa Sudan mwaka 2011.