Watu 8 wauawa kinyama huko Tanga, Tanzania

Image caption Tanga,Tanzania

Wakaazi wa kijiji cha Kibatini katika eneo la Tanga Kaskazini mwa Tanzania wamewachwa na mshtuko na hofu baada ya watu wanane kukatwa vichwa.

Lengo la mauaji hayo halijulikani na maafisa wa polisi wanawasaka waliotekeleza kitendo hicho ambao wanadaiwa kujificha katika msitu uliopo karibu.

Pia wamewataka wakaazi kuwa na subra huku wakiendelea na uchunguzi lakini familia nyingi zimetoroka kijiji hicho kufuatia shambulio hilo.

Abushiri anayeishi Kibatini na ambaye alipoteza nduguye wakati wa shambulio hilo anasema kuwa serikali inahitaji kufanya zaidi ili kuwalinda wakaazi.

''Kijiji chetu kina nyumba 30 pekee na hakuna amani,kutakuwa na amani wakati washukiwa wa vitendo hivi watakamatwa,kushtakiwa na kufungwa jela''.

Vikosi vya usalama vimepelekwa katika eneo hilo.