Je,watu wanasemaje kuhusu Muhammud Ali?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption George Foreman

George Foreman:Aliyekuwa mwanamasumbwi George Foreman aliyewahi kupambana na Mohammed Ali katika mechi iliofanyika Zaire kabla ya Ali kuibuka mshindi anasema kuwa Mohammed ali alikuwa na ushawishi wa kukufanya akupende.Iwapo usingempenda angekufanyia vituko zaidi ndio uweze kumchukia zaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Floyd Mayweather

Floyd Mayweather Jr:Leo moyo wangu unanung'unika kwa kumpoteza mwanzilishi ,bondia hodari,bingwa na shujaa kwa vyovyote vile.Hakuna siku niliingia katka ulingo wa ndondi bila kukukumbuka ,alisema katika mtandao wa instagram.Ucheshi,uzuru wako na vyenginevyo ndio vitu tutakavyovienzi.

Odesa Grady Clay:Kila mara nilihisi Mungu alimfanya Muhammad kuwa mtu muhimu,lakini sijui kwa nini mungu alinichagua mie kumbeba mwana huyu.wakati alipokuwa mtoto hakuweza kutulia.alitembea na kuzungumza na kufanya kila kitu wakati wake.Akili yake ilikuwa kama upepo unaovuma na kueleka kila sehemu.

Rahman Ali: Ndguye Mohammed Ali anasema kuwa marehemu alikuwa akimtaka amrushie mawe,nilidhani ameshikwa na wazimu,lakini mawe hayo angeyahepa yasimpige...sikuweza kumpiga.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Malcolm X

Malcom X: Ndio mwanariadha hodari mweusi niliyewahi kumjua na ana umuhimu mkubwa kwa watu wake.Kwa sababu mabilioni ya watu kutoka Afrika,Asia na Arabia wanakupenda lazima ujue majukumu yako.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jesse Jackson

Jesse Jackson:Walikataa kusikiza ushuhuda wake kuhusu dini yake.Walijaribu kumnyanyasa ,walijaribu kumuathiri kimwili na kiakili