UM kupeleka misaada zaidi nchini Syria

Haki miliki ya picha
Image caption Magari ya misaada nchini Syria

Maafisa wa kibalozi jijini New York wanasema kuwa hiyo kesho Umoja wa Mataifa utaomba rasmi Serikali ya Syria kuruhusu kudondosha vyakula na madawa katika maeneo wanakoishi wananchi walio katika hatari ya kufa kutokana na ukosefu wa chakula.

Lakini mwandishi wa BBC katika Umoja wa Mataifa anasema kuwa dalili za awali kutoka kwa Serikali ya Syria ni kuwa huenda idhini hiyo isitolewe.

Kati ya maeneo 17 yanayokabiliwa na vita Serikali ya Rais Bashar Al Assad imetoa idhini kwa maeneo 12 pekee na idhini nusu kwa maeneo matatu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu walioadhirika na vita vinavyoendelea nchini Syria

Uingereza ilisema idhini hiyo imetolewa kama imechelewa na kwa kiasi kidogo mno. Ufaransa ilitaja hatua hiyo kama tone kwenye Bahari.