Guinea Bissau na Ghana zafuzu kwa kombe la Afrika

Image caption Kikosi cha Guinea Bissau.

Guinea Bissau ikefuzu kwa kombe la taifa bingwa abarani Afrika kwa mara ya kwanza kabisa.

Bada ya kuwashinda Zambia siku Jumamosi, nafasi yao katika kinyanganyiro hicho cha mwaka ujao ilidhihirika wakati Congo-Brazzaville walipoteza mwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Kenya.

Ghana ilifaulu kufuzu baada ya kushinda ugenini kwa mabao mawili wa bila dhidi ya Mauritius.