Ndege zashambulia wapiganaji Allepo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege zashambulia mji wa Allepo

Ripoti kutoka Syria zinaeleza kuwa ndege zimefanya mashambulio kadha, dhidi ya mitaa ya wapiganaji katika mji wa Aleppo.

Wafanya kazi za uokozi wamenukuliwa wakisema, kuwa miili kama 20 imetolewa kwenye kifusi katika maeneo kadha.

Pia kuna taarifa kwamba maeneo ya mji huo yanayodhibitiwa na serikali, yameshambuliwa kwa makombora kutoka upande wa wapiganaji.

Shirika la habari la taifa limesema watu kama 24 waliuwawa jana, katika mashambulio kama hayo.