Upepo mkali, mvua na mafuriko vyaikumba Australia

Haki miliki ya picha AFP

Mwambao wa mashariki wa Australia umepigwa na pepo kali, mvua nyingi na mafuriko.

Majimbo ya New South Wales, Victoria, Queensland na Tasmania, yameathirika sana.

Mamia ya watu wamekosa umeme, na amri imetolewa kwa baadhi ya watu kuhama makwao.

Sehemu ya uwanja wa ndege wa Sydney ilifungwa, kwa sababu ya upepo mkali.