Shughuli ya upigaji kura yaendelea Peru

Haki miliki ya picha getty

Watu nchini Peru wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa wagombea wote wawili, Keiko Fujimori na Pedro Pablo Kuczynski, karibu wako sare katika uchaguzi wa leo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Keiko Fujimori

Bibi Fujimori, wa mrengo wa kulia, aliongoza katika duru ya kwanza mwezi Aprili.

Lakini Bwana Kuczynski, aliyewahi kufanya kazi katika Benki ya Dunia, naye amesonga mbele.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pedro Pablo Kuczynski

Bibi Fujimori ni mtoto wa rais wa zamani, Alberto Fujimori, ambaye amefungwa kwa kutenda uhalifu dhidi ya binaadamu.

Amesema swala muhimu ni kupambana na uhalifu.

Bwana Kuczynski anasema, atatumia uzoefu wake katika uchumi wa kimataifa, kuchangamsha uchumi wa Peru uliozorota.