Rais wa Nigeria kutibiwa London

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Nigeria kutibiwa London

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amechukuwa likizo ya siku 10 ilikupata matibabu maalum nchini Uingereza.

Msemaji wa rais , amewaambia waandishi wa habari kuwa Buhari atatumia fursa ya likizo yake huko London kupata matibabu maalum ya sikio.

Uthibitisho huo unafuatia habari zilizochapishwa jumamosi na gazeti moja nchini humo Premium Times kuwa rais Buhari ni mgonjwa na hilo ndilo lililomsababisha asihudhuria hafla ya kuzindua usafishaji wa mazingira ya eneo la kuzalisha mafuta la Niger Delta.

Image caption Uthibitisho huo unafuatia habari zilizochapishwa jumamosi na gazeti moja nchini humo Premium Times

Kwa mujibu wa msemaji huyo rais Buhari ametibiwa nchini Nigeria, lakini madaktari wake wameshauri kuwa rais huyo afanyiwe uchunguzi zaidi, kama hatua za tahadhari.

Tangazo hilo limetolewa siku chache baada ya rais Buhari, kuhairisha ziara yake katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta.