Pedro aongoza katika matokeo ya awali Peru

Haki miliki ya picha Getty

Matokeo yasio ramsi ya uchaguzi wa urais nchini Peru yamebainisha kuwa aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa benki ya dunia, Pedro Pablo Kuczynski, anaongoza kwa idadi ndogo ya kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Keiko Fujimori.

Kura ya maoni kabla ya uchaguzi huo, ilimpa Bi Fujirmori uongozi mkubwa lakini waandishi wa habari wanasema kuwa kashfa za ufisadi ndani ya chama chake huenda zimehujumu uungwaji mkono wake.

Bi Fujimori ni mwana wa kike, wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Alberto Fujimori ambaye yuko gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Naye bwana Kucyinski ameshutumiwa kutokana na uhusiano wake na wafanyabiashara mashuhuri nchini humo.