Wakamatwa kwa kuuza figo kiharamu India

Haki miliki ya picha AFP

Polisi nchini India wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa kiongozi wa kundi linaloendesha biashara ya figo za binadamu kinyume na sheria katika moja ya hospitali maarufu ya kibinafsi nchini humo.

T Rajkumar Rao, aliakamatwa katika hospitali ya Kolkata siku ya Jumanne.

Polisi wanasema kuwa aliongoza genge ambalo liliwahadaa watu maskini kuuza figo zao, ambazo baadaye ziliuzwa kwa faida kubwa.

Watu wanane wakiwemo wafanyikazi watano wa hospitali ya Apollo walikamatwa awali kuhusiana na suala hilo.

Hospitali hiyo imekana kuhusika katika biashara hiyo haramu, ikisema kuwa imekuwa muathiriwa wa visa vya kuwadanganya wagonjwa .