Rais wa India kuzuru Afrika

Rais Pranab Mukherjee

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Rais Pranab Mukherjee

Rais wa India Pranab Mukherjee, anaanza ziara ya siku sita barani Afrika yenye lengo la kuboresha ushirikiano wa kibiashara.

Atatembelea Ghana, Ivory Coast na Namibia.

Afrika inatambuliwa kama mzalishaji muhimu wa mafuta na madini yanayohitajika na sekta ya kiviwada inayopanuka nchini India.

India pia ina lengo la kuboresha uhusiano ambao tayari umejengwa kati ya China na nchi za Afrika.

Afisa mmoja nchini India alizitaja nchi hizo tatu ambazo rais wa India atazizuru, kama zilizo na demokrasia iliyokomaa na dhabiti.