Microsoft kununua Linkedln kwa dola bilioni 26

Haki miliki ya picha Getty

Kampuni ya Microsof imetangaza kuwa itanunua mtandao wa taaluma wa Linkedln kwa kima cha dola bioni 26.

Inaamika kuwa ununuzi huo utasaidia Microsoft kuongeza mauzo ya biasaara yake na programu zake za emali na pia kupenya kwenye mtandao mkubwa zaidi wa taaluma duniani.

Linkedln ina zaidi ya wanachama milioni 430 kote duniani.

Microsoft ilisema kuwa Linkedln itaendelea kudumisha tamaduni na uhuru wake.