Wizi wa parachichi washuhudiwa New Zealand

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Parachichi

Kumeshuhudiwa upungufu mkubwa mno wa zao la parachichi nchini New Zealand, kufuatia mavuno duni msimu huu.

Hatua hiyo imesababisha wizi mkubwa wa matunda hayo ambapo wezi wanavamia mashamba machache yanayonekana kuwa na zao hilo.

Wizi mkubwa umeshuhudiwa katika maeneo ya Carloads kaskazini mwa nchi hiyo, huku serikali ikitangaza kuwa itatoa ulinzi mkali.