Microsoft kushiriki biashara ya Bangi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Microsoft kushiriki biashara ya Bangi

Kampuni ya kutengeza programu za kompyuta Microsoft, imekuwa ya hivi karibuni zaidi kujiunga na biashara ya bangi katika majimbo kadhaa nchini Marekani yaliyohalalisha uvutaji wa bangi.

Kampuni hiyo kubwa imeungana na kampuni nyingine ya "Kind Financial - inayotengeneza programu za kusaidia idara za serikali zinazodhibiti uzalishaji na mauzo ya bangi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kind Financial imekuwa ikiuza programu zake kwa idara za usalama zinazofuatilia ukuzaji uuzaji na usambazi wa bangi

Yamkini Microsoft inasema kuwa uhusiano wake na kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko Carlifornia ni wa ''kipekee''

Kind Financial imekuwa ikiuza programu zake kwa idara za usalama zinazofuatilia ukuzaji uuzaji na usambazi wa bangi kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Haki miliki ya picha TWITTER
Image caption Microsoft imeungana na kampuni nyingine ya "Kind Financial

Programu hiyo ya Kind inaitwa ''Agrisoft Seed to Sale, " na inawaunganisha wakulima wa bangi wauzaji idara zinazosaidia kudhibiti matumizi ya bangi serikali na na sekta ya fedha.

Majimbo kadhaa nchini Marekani yameruhusu uuzaji wa bangi kwa matumizi ya kimatibabu na kujistarehesha, japo imeharamishwa chini ya sheria kuu za nchi hiyo.