Iran kununua ndege 100 kutoka Boeing

Haki miliki ya picha AirTeamImages

Mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Iran imetangaza kuwa itanunua ndege 100 kutoka kampuni ya uundaji ndege ya Boeing, nchini Marekani.

Mwezi Februari, Marekani iliipa idhini kampuni ya Boeing kuanzisha mazungumzo ya kibiasahara na Tehran, kufuatia kuondolewa japo kwa kiasi kidogo vikwazo vya kiuchumi, baada ya makubaliano ya kupunguza mpango wake wa kinuklia.

Iran inajikakamua kununua ndege mpya za kibiashara, kuchukua mahala pa ndege zake nzee ili kupanua sekta yake ya uchukuzi wa angani.

Mwezi Januari, Iran iliafikia makubaliano na Marekani kununua zaidi ya ndege 100 kutoka katika kampuni ya uundaji wa ndege barani Ulaya, ya Airbus.

Siku ya Alhamisi, mamlaka barani Ulaya iliamua kuondoa marufuku katika orodha yake ya uchukuzi wa angani ndege za Iran Air, iliyokuwa imewekwa hapo awali kwa sababu za kiusalama.