Kura ya maoni Uingereza ni wiki hii

Kura ya maoni Uingereza ni wiki hii

Leo BBC inaanza mfululizo wa ripoti tulizokuandalia kuelekea kura ya maoni ya Uingereza Alhamisi hii itakayo amua iwapo taifa hilo lijitoe au lisalie katika Umoja wa Ulaya.

Huku siku tatu zikiwa zimesalia kufikia siku ya upigaji wa kura ya maoni zinaonyesha mchuano unatarajiwa kuwa mkali.

Lakini kura hii ya maoni ina maana gani kwa uhusiano wa Uingereza na bara la Afrika?Regina Mziwanda amezungumza na mwandishi wa BBC, Zawadi Machibya kutoka London akitaka kujua umuhimu wa kura hiyo ya maoni