Roma Italia yamchagua mwanamke wa kwanza meya

Haki miliki ya picha .
Image caption Meya mpya wa jiji la Roma Italia Virginia Rajji wa vuguvugu la 5 Star

Wapigaji kura katika mji mkuu wa wa Roma nchini Italia, wamemchagua mwanamke wa kwanza kuwa meya wa mji huo.

Virginia Rajji wa vuguvugu la 5 Star, amemshinda mpinzani wake Roberto Giachetti katika kura ya marudio.

Bwana Giachetti, ni mfuasi wa chama cha demokrasia cha mrengo wa kati-kushoto, chake waziri mkuu wa bw Matteo Renzi, ambacho pia kilipoteza kiti cha umeya katika mji wa Turin, huku wagombea wa chama chao wakishinda viti vya umeya katika miji ya Milan na Bologna.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Virginia Rajji wa vuguvugu la 5 Star, amemshinda mpinzani wake Roberto Giachetti katika kura ya marudio.

Bi Rajji, ambaye aliendesha kampeini yake akiahidi kukabiliana na ufisadi na kuwasaidia wasiojiweza katika jamii, amesema kuwa ushindi wake ni mwanzo wa enzi mpya ya uongozi nchini Italia.