Rwanda na mpango kabambe kwa waja wazito

Rwanda na mpango kabambe kwa waja wazito

Je unajua kwamba ujumbe wa simu za rununu unaweza kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa? Katika juhudi za kuimarisha afya ya kinamama na watoto nchini Rwanda kuna mpango kabambe wa kumfwatilia mama mja mzito na kuripoti afya yake kwa kutumia ujumbe wa simu za mkononi.Mpango huo unaofahamaika kama <<Rapid SMS >> umesifika kwa kupunguza vifo vya maelfu ya watoto kwa kiwango cha kuridhisha.

Vifo vingi vya kinama wajawazito hutokana na kuwa wengi hujifungua nyumbani au barabarani kwa kushindwa kufika hospitali,lakini mfumo huu ulioanzishwa mwaka 2009 ulisaidia kinamama kufikishwa hospitali ama katika zahanati.

Nchi nzima kuna washauri wa afya ya uzazi wapatao elfu 45.wanateuliwa na wananchi na kupewa mafunzo ya msingi ya kusaidia katika masuala ya afya.

Ripoti ya benki ya dunia imeiorodhesha Rwanda miongoni mwa mataifa yenye kupiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa.Takwimu za mwaka jana kutoka banki ya dunia zimebainisha kuwa vifo vya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja vilikuwa 31 kwa watoto elfu moja,idadi iliyo chini kabisa ya wastani wa dunia ya watoto 31,7 wanaofariki.

Yves BUCYANA ana maelezo zaidi, karibu usikilize.