Hong Kong kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu

Serikali ya Hong Kong inasema itapiga marufuku kabisa biashara ya pembe za ndovu ndani ya miaka mitano inayokuja.

Maafisa wamesema kuwa hawana mipango ya kuwafidia wafanyibiashara wa pembe za ndovu.

Kwa sasa aina fulani ya pembe ni halali kuuzwa lakini makundi ya kutunza wanyama yanaamini kuwa hii inachangia kunoga kwa biashara ya pembe za ndovu.

Shirika linalohusika na wanyamapori duniani linasema linaamini kuwa marufuku hiyo itatekelezwa ndani ya miaka miwili.