Muhimu kuhusu uchaguzi wa Tanzania 2010

Takwimu muhimu za uchaguzi

Idadi ya wakazi: milioni 42 (Benki ya Dunia 2008) Watu waliojiandikisha kupiga kura: milioni 19 (Tume ya Uchaguzi Tanzania) Siku ya Kupiga Kura: Tarehe 31 Oktoba 2010 Mwisho wa Kampeni: Tarehe 30 Oktoba 2010 Idadi ya Wagombea Urais: 07 Majimbo ya Ubunge: 239 Urefu wa Muhula: Miaka mitano

Tanzania ilifanya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, baada ya kufanya mabadiliko ya katiba mwaka 1992.

Katika uchaguzi huo mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Benjamin Mkapa aliandika historia kwa kuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kwa kura katika uchaguzi ulioshirikisha wagombea na vyama vingi.

Aliwashinda wagombea wengine kama vile Augustine Mrema, Profesa Ibrahim Lipumba (ambaye anagombea kwa mara ya nne mwaka 2010) na Freeman Mbowe (mwenyekiti wa CHADEMA aliyeamua kumpisha Dr Wilbrod Slaa katika uchaguzi wa 2010).

Mwaka 2000, Rais Mkapa alirejea tena madarakani kwa muhula wake wa mwisho na akafanikiwa kuwaangusha wagombea wa vyama vya upinzani. Muda wake ulimalika mwaka 2005.

CCM walianza upya mchakato wa kura za maoni ndipo alipopatikana Jakaya Kikwete, aliyeingia madarakani kwa ushindi uliotajwa kuwa wa kishindo.

Mwaka 2010, Rais Kikwete anachuana na wagombea sita akiwemo Profesa Ibrahim Lipumba aliyeshiriki kila uchaguzi tangu mwaka 1995.

Wagombea Urais wa Muungano mwaka 2010

  1. Jakaya Kikwete – CCM (aliyeko madarakani)
  2. Dr Wilbrod Slaa – CHADEMA
  3. Prof Ibrahim Lipumba ( anagombea kwa mara ya nne)
  4. Hashim Rungwe – NCCR Mageuzi
  5. Peter Mziray – APPT
  6. Fahma Dovutwa – UPBP
  7. Mutamwega Mugahiwa -TLP

Kwa upande wa visiwani Zanzibar, uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi pia ulifanyika mwaka 1995 wakati Salmin Amour wa CCM, alipotangazwa mshindi katika uchaguzi uliokuwa na matatizo na utata. Tayari alishakuwa madarakani wakati uchaguzi ukifanyika, na baada ya ushindi huo akamalizia muhula wake wa Rais wa Zanzibar.

akimwangusha Maalim Seif Shariff Hamad ( ambaye 2010 anagombea kwa mara ya nne).

Wagombea Urais wa Zanzibar 2010

Seif Shariff Hamad – CUF

Dr Ali Mohammed Shein - CCM Juma Ali Khatib - TADEA Haji Ambar Khamis - NCCR-Mageuzi Said Soud Said – AFP Haji Kitole – SAU