Hofu ya vita wiki moja kabla Uhuru

Hata kabla ya Sudan ya kusini kutangaza kuwa Taifa huru wiki hii, tayari nchi hiyo inakabiliana na zaidi ya makundi sita ya wapiganaji walioasi.

Image caption Nguvu ya waasi

Kwenye picha ya video iliyo mikononi mwa BBC, mamiya ya wapiganaji kutoka kusini mwa Sudan wanaonekana wakifanya mazowezi ya kijeshi kwa kuimba na kujaribu silaha zao mpya.

Haki miliki ya picha ap
Image caption Tabasamu za viongozi

Sura za tabasamu zinazojitokeza kwenye video hii ni kinyume kabisa na ukweli wa matayarisho ya vita vikali. Makundi haya ya waasi yamepigana mara kadhaa na jeshi la kusini, na ni tishio kubwa kwa utulivu wa Taifa hili changa.

Vishawishi vilivyosababisha waasi kuasi serikali yao ni vingi, lakini wengi wa viongozi wao waliwahi kuwa maofisa wakuu katika vikosi vya kusini,Sudan People's Liberation army(SPLA), au hata viongozi wa mgambo waliopambana na serikali ya Sudan kwa kipindi cha miaka 21 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyomalizika kwa amani ambayo imewezesha Uhuru wa sehemu ya kusini.

Image caption Peter Gadet wa SSLA

Mojapo ya makundi hayo ya waasi, lijulikanalo kama South Sudan Liberation Army(kifupi -SSLA) likiongozwa na Peter Gadet linadai kuwa linapiga vita rushwa, ukosefu wa maendeleo na umiliki wa nyadhifa unaofanywa na kabila la Dinka.

Makabila ya Dinka ndiyo kabila moja kubwa kuliko yote ya Sudan ya kusini, na linalaumiwa kwa kushikilia nyadhifa nyingi muhimu katika jeshi la kusini pamoja na serikalini.

Kiwango kikubwa cha fedha hutumika kwa gharama za jeshi ikiwa ni robo ya mapato ya Sudan ya kusini, vilevile ni sawa na mara tatu ya jumla ya fedha zinazotumiwa kwa huduma ya Afya na Elimu kwa pamoja.

Kwa kifupi, hii ni sehemu tu ya wasiwasi unaoikabili serikali mpya wa makundi ya waasi pamoja na maadui wa kale katika utawala wa Sudan ya kaskazini huko Khartoum.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ushauri lipunguzwe nusu

Ingawaje pesa nyingi hutumiwa kwa mishahara ambapo afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyeko Sudan ya kusini, David Gressley alinena hivi karibuni akishauri kuwa bora jeshi lipunguzwe kwa nusu baada ya Uhuru.

Mkono wa kaskazini upo?

Wapiganaji wa kundi la SSLA wamepambana na SPLA mara kadhaa karibu na makao yao makuu katika Jimbo la Unity.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais al Bashir

Kwa mujibu wa SPLA, makundi yote yanafanana kwa kitu kimoja;Yote yanadhaminiwa na aliyekuwa adui yao wote aliye mjini Khartoum.

Video iliyotoa sura ya hali ya mambo ilivyo huko Kusini mwa Sudan ilikabidhiwa kwa BBC na kiongozi wa waasi ambaye wakati huo alikuwa mjini Khartoum.

Ikiwa kuna ukweli au hata kama hapana ukweli, serikali ya Sudan ya kusini inaonelea kila hatua ya njama inayofanywa na wakuu wa Khartoum na yote haya yakiashiria uhusiano mbovu baina yao.

Katika kipindi cha vita vya miongo miwili, eneo la kaskazini lilikuwa na tabia ya kuyapa silaha makundi yanayohasimiana ili kulilegeza jeshi la SPLA.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Riek Machar

Hata Makamu wa Rais wa Sudan ya kusini, Riek Machar wakati mmoja alijitenga kutoka SPLA.

Hata hivyo Chama cha NCP cha Rais Omar al-Bashir kinakanusha kuwa kinaunga mkono kizazi kipya cha makundi ya waasi.

"Peter Gadet na wengine kama yeye hawakuwa sehemu ya Chama cha Rais Bashir cha NCP wala jeshi la Sudan, alikuwa ni sehemu ya mgambo wa SPLA, walioasi kufuatia kuibia kura baada ya Uchaguzi mkuu wa Sudan ya kusini, kwa mujibu wa afisa wa Chama cha NCP Ibrahim Ghandour.

Habari zisizokuwa za kufurahisha ni kwamba waasi hao wanapanga kutumia silaha zao kabla au baada ya sherehe za Uhuru wa Sudan ya kusini.