Huwezi kusikiliza tena

Kiswahili Libya

Libya ni miongoni mwa nchi ambayo kwa zaidi ya miongo miwili imekuwa ikifundisha lugha ya kiswahili katika baadhi ya vyuo vyake hasa Chuo Kikuu cha Sebha.

Kufundishwa kwa lugha ya kiswahili nchini Libya, kumetoa fursa ya ajira kwa watu mbali mbali wa mataifa ya Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Kenya ambao hutumiwa kama walimu wa lugha hii.

Dk. Peter Mtesigwa ambaye ni mmoja wa wahadhiri huko nchini Libya anamwelezea mwandishi wetu Aboubakar Famau kutoka Dar es Salaam jinsi Libya ilivyopiga hatua katika kueneza lugha ya Kiswahili.