China: Je ndio nchi inayoongoza kwa werevu duniani?

Image caption Watoto wa shule nchini China

Matokeo ya china katika mitihani ya kimataifa shuleni, ambayo haijawahi kuchapishwa, ni ya kuridhisha saana. Hii ni kauli ya Andreas Schleicher, ambaye anahusika na mitihani ya kimataifa ya Pisa.

Mitihani hii hufanywa baada ya kila miaka mitatu na kuandaliwa na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo. Lengo lake huwa ni kuchunguza uwezo wa mtoto kusoma, kufanya hesabu na sayansi.

Mitihani ya Pisa, imetumika kama kigezo cha kimataifa kwa wanafunzi kote duniani.

Matokeo haya yanaonyesha kuwa China ina mfumo wa elimu ambao unapiku nchi za magharibi.

Licha ya wengi kupiga darubini sana hali ya kiuchumi na kisiasa nchini China, ripoti hii inatoa fursa kwa watu kuona nchi hiyo inavyoelimisha kizazi kijacho.

Wanajizatiti sana.

Mitihani ya Pisa mwaka 2009, ilionyesha wazi kuwa Shanghai ilikuwa juu kwenye orodha ya waliofanya vyema kielimu kimataifa.

Hata hivyo haikuwa wazi ikiwa Shanghai pamoja Hong Kong ambayo pia ilifanya vizuri sana, ziliwakilisha ipasavyo kikanda au kulikuwa na maeneo mengine ambayo yalifanya vizuri zaidi. .

Bwana Schleicher anasema kuwa matokeo ambayo hajachapishwa yanaonyesha kwa wanafunzi katika maeneo mengine ya China pia wanafanya vyema sana.

Image caption Andreas Schleicher " Inategemea nafasi wanayopewa wanafunzi kufanikiwa maishani"

"Hata katika maeneo ya vijijini na maeneo yaliyotengwa kiuchumi, ni wazi kuwa wanafunzi wana bidii sana" alisema Schleicher.

Aliongeza kuwa matokeo ya mitihani yanaonyesha wanafunzi wanajizatiti sana kuweza kufanikiwa licha ya mazingira magumu sawa na pengo lililoko kati ya wanafunzi kutoka familia maskini na zile tajiri.

Bwana Schleicher alielezea kushangazwa zaidi na matokeo ya shule za vijijini ikilinganishwa na alichoshuhudia mijini kama vile Shanghai. Yaani hali wanavyojizatiti wanafunzi ni ya kutia moyo.

Nchini China msingi wa maisha bora ni elimu, na kulingana na utafiti huo hilo lilibainika wazi kwani wanafunzi wanaelewa kuwa bila elimu, maisha yako hayatakuwa mazuri.

Matokeo ya wanafunzi wanaotoka famailia zisizojiweza nchini China, bila shaka inaweza kuonewa wivu na nchi za magharibi kulingana na bwana Schleicher.

Katika juhudi zake kupata picha halisi, mitihani ilifanywa katika mikoa tisa ikiwemo katika maeneo yenye viwango vya juu vya umaskini, katika maeneo yenye kipato cha kadri na mwishowe katika maeneo yenye matajiri wengi.

Wanafunzi wa shule ya upili ya Nanjing wanafahamu vyema kauli mbiu yao " lazima niende katika chuo kikuu" walisika wakisema nje ya shule yao.

Hata hivyo serikali ya China imekataa kuruhusu kuchapishwa kwa matokeo ya mitihani hiyo.

Lakini bwana Schleicher anasema kuwa matokeo hayo yanaonyesha picha halisi ya jamii kuekeza kwa ujumla katika elimu.

Haki miliki ya picha bb
Image caption Wanafunzi nchini China

Katika ziara yake katika mkoa mmoja, bwana Schleicher anasema aliona majengo ya shule yakiwa yanapendeza sana.

Katika nchi za magharibi, ungedhani majengo hayo ni maduka ya kifahari.

Pia kulikuwa na tofauti kubwa kati ya wanafunzi vijana, walioulizwa kwa nini wanadhani wanafunzi wanafaulu sana shuleni.

Raia kutoka Marekani husema ni bahati tu , ni mtu kuzaliwa akiwa ana akili ya kujua mfano hesabu na ikiwa hiyo nidio maoni ya wengi wanafunzi huonelea ni bora kufanya anachoona anaweza mwenyewe.

Barani Ulaya elimu ni juu ya urithi, mfano wanafunzi husema babangu alikuwa seremala kwa hivyo na mimi nitakuwa seremala, haoni haja ya kufanya bidii kusoma.

Nchini China wanafunzi wengi husema inategemea bidii yangu, ikiwa nitafanya bidii bila shaka nitafanikiwa masiahani.