Watu wasioona wanavyotalii dunia

Haki miliki ya picha b
Image caption Emma Tracey hawezi kuona lakini alitembelea hifadhi ya wanyama pori nchini Kenya.

Msanii wa kijerumani Christian Jankowski alitembelea vivutio vya utalii mjini Dubai kupitia mpango utamaduni ulioandaliwa na BBC. Lakini inakuwa vipi kwa watu wasioona wanaposafiri nchi za nje? Anauliza Emma Tracey mtengeza kipindi cha Ouch cha BBC katika blog ya walemavu na kipindi cha majadiliano.

Hali ya kutokuona toka kuzaliwa, wazo la kutalii kwa kweli ni geni kwa upande wangu, kusimama katika mtaa kuangalia majengo ya kihistoria, haivutii kwa upande wangu.

Lakini bado napenda kwenda kutembea kutoka maisha ya kukaa mahali pamoja kila siku na kujifunza utamaduni mpya kwa kwenda safari za utalii.

Nilipata wakati mgumu wakati nikisafiri kwenda Machu nchini Peru, ni muhimu kuchagua sehemu inayofaa kusafiri.

Kiasi cha msaada nilichokuwa nahitaji wakati wa kupanda mlima kufika kileleni kilininifanya kuchagua maeneo yanayofaa zaidi.

Sasa zafari zangu za utalii zinaonekana kuwa katika maeneo ya miji mikubwa yenye kelele, yenye mfumo mzuri wa usafiri na maarufu kwa vyakula vizuri na watu wakarimu.

Mara nyingi nasafiri pamoja na familia au marafiki, lakini hiyo si njia pekee inayopatikana kwa watu wasioona.

Mkufunzi wa masuala ya teknolojia na mtu mashuhuri kwa kusafiri duniani Robbie Sandberg anapendelea kusafiri peke yake.

Image caption Mtalii asiyeona

"ingawaje inaweza kunichukua muda mrefu kufika sehemu ninazokusudia, ninaweza kufanya kulingana na muda wangu, na hayo ni mafanikio''. Anasema. Robbie Sandberg anasema hupata vielelezo vya safari kupitia bar za maeneo husika.

Ikiwa wanasafiri na watu wengine au peke yao, wasafiri watalii wasioona wanaonekana kujenga picha ya hisia ya mahali kwa kutumia vitu vingine. Hili ni jambo ambalo Sandberg anakumbuka kulifanya katika safari ya hivi karibuni ya Kerala nchini India.

"Wenyeji wachache walizungumza Kiingereza, kwa hiyo ilikuwa ni vigumu kuomba msaada. Nilitambua hali ya joto na kuhisi barabara niliyokuwa nikikanyaga ukichukulia kuwa hazikuwa na sehemu za waendao kwa miguu.

''Ilikuwa ni sauti za vijipikipiki zilizokuwa zikizunguka zilizosaidia kunipa mwelekeo. Kisha nitaelekea pembezoni kupata harufu ya bahari na samaki waliovuliwa na niliweza kujiweka sawa.

Image caption Christian Jankowski

Daima huwa ni jambo rahisi kwa watu wasioona kufikia eneo husika, kwani kupata msaada wa bure, kutoka lango la kiwanja cha ndege, na kuingia na kutoka katika ndege na kisha kwenye usafiri mwingine, hupatikana katika nchi nyingi. Lakini inapotokea upo katika eneo usilolifahamu inaweza kuwa ni changamoto.

James Holman, au maarufu kama anavyojulikana Msafiri Asieona, alijipatia umaarufu kwa kuwa mtu asieona wa kwanza kusafiri kuzungunguka dunia katikati ya karne ya 19.

Mwaka 1822 safari yake ilikatiziwa nchini Urusi wakati aliposhukiwa kuwa mpelelezi na kutupwa gerezani. Mwanajeshi huyo wa zamani aliendelea na safari yake mara baada ya kuachiliwa na kuimaliza mwaka 1832.

Alisemekana kuweza kutambua njia yake kwa kutumia njia ya kukusanya vielelezo vya mazingira yake kupitia kusikiliza mlio wa ufito wake wa mwanzi.

Lakini baadhi ya watu wamekuwa na mashaka kuhusu ukweli wa habari zake. Hadi anakufa, Holman alikuwa karibu kusahaulika, na kitabu kinachoelezea maisha yake hakikuwahi kuchapishwa.

Amar Latif ni mmiliki wa kampuni ya kuratibu safari za utalii ya Traveleyes, ambayo inaratibu safari za mchanganyiko kwa wasioona na wanaoona. Kampuni hiyo inampangia kila msafiri asiyeona kuwa na mtu tofaouti anayeoona kila siku, ambaye humuelezea asiyeona yaliyopo katika mazingira husika.

Haki miliki ya picha b
Image caption Robbie Sandberg

Akiwa haoni yeye mwenyewe, Latif anasema kupangiwa mtu anayeoona inasaidia sana kufurahia safari kujua yanayomzunguka. Lakini kwa safari kuweza kuwa ya mafanikio, asiyeona lazima aweze kufurahia sawa na yule anayeona au kumuongoza.

"Nisingependa kusafiri, badala yake ningependelea kwenda sehemu kama Zimbabwe ambako unaweza kuhisi uwepo wa wanyama," anasema. ''Niligusa simba kule, hata kuhisi nyuso zao.''

Katika nchi ambazo wenyeji hawajazoea kuwa karibu na wasioona, Latif anashauri kufanya kazi ya ziada. Anasema kuwa ni muhimu kufahamu hasa ni nini unataka kufanya ukiwa pale, na kijifunza vya kutosha jinsi ya kuzoeana na wenyeji na kuwafanya wakuzoee.

Nimegundua kuwa hii ni njia nzuri pia ya kuwa na uhuru binafsi unapokuwa safarini. Napanga kwa uangalifu na kushikilia nafasi zote za safari yetu na kusoma maelezo ya eneo husika ili kumpasha yule ninayesafiri naye vitu vizuri vya kutokukosa tutakavyokutana navyo tukiwa safarini.