Aina mpya ya binadamu wa kale Kenya

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption hominid

Kwa mujibu wa ushahidi wa visukuku vilivyopatikana Kaskazini mwa Kenya kuna aina mpya ya binadamu walioishi huko takriban miaka milioni mbili iliyopita, wamesema wataalamu.

Uvumbuzi huu unaibua hisia kuwa aina tatu za viumbe waliishi kwa wakati mmoja barani Afrika. Utafiti huu unaongezea ushahidi mwingine ambao haukubaliani na dhana maarufu kuwa asili ya mwanadamu wa leo alitokana na nyani.

Utafiti huu umechapishwa kwenye jarida la Nature.

Wana athropolojia ama wataalamu wanaotafiti masuala ya kale wamegundua mabaki au visukuku(fossils) vya binadamu vyenye umri wa miaka iliyo kati ya milioni 1.78 na milioni 1.95. Visukuku hivi ni vya uso ukiwa na mifupa ya taya miwili ikiwa na meno yake.

Natural History Museum, London Ugunduzi huu unakubaliana na mtazamo kuwa fuvu lililopatikana mnamo mwaka 1972 lilikua la aina ya binadamu tofauti anayejulikana kama Homo rudolfensis. Fuvu hili lililkua tafauti na mengine ya nyakati hizo na haikua rahisi kubaini kama kiumbe huyu alikua na tafauti au ni kiumbe tofauti wa aina mpya ya viumbe.

Image caption Mafuvu mapya

Kwa kipindi cha miaka 40 fuvu hili ndiyo mfano pekee uliokuepo wa kiumbe kwa hiyo haikua rahisi kubaini kama kiumbe huyu alikua wa kipekee au mmoja wa viumbe wapya.

Kwa ugunduzi wa visukuku wapya watatu wataalamu sasa wanaweza kusema bila kusita kwamba H.rudolfensis kweli alikua aina tofauti ya kiumbe binadamu aliyeishi takriban miaka milioni mbili iliyopita sambamba na aina nyingine za binadamu.

Kwa mda mrefu babu wa binadamu aliyefahamika alidhaniwa kua aina kutoka nyani, wanaodhaniwa kua waliishi miaka milioni 1.8 iliyopita wakijulikana kama Homo erectus. Walikua na vichwa vyembamba, nyusi zilizotanda na walisimama wima.

Lakini miaka 50 iliyopita, wataalamu waligundua mifano iliyoishi kabla ya hapo na iliyoishi kama nyani ikijulikana kama Homo habilis ambayo huenda iliishi wakati mmoja na H.erectus. Ushahidi wa sasa unaonyesha kua wakati huo H. rudolfensis alikuepo pia na kuleta dalili za kua huenda ikawa aina nyingine ya binadamu waliishi wakati huo.

Uvumbuzi wa sasa ni ushahidi unaozidi kufuta dhana ya kwamba sisi tulianza mwendo wa kubadili maumbile yetu kutoka nyani anayekwenda kwa kujikongoja taratibu hadi tulipoinuka kusimama kama binadamu wa leo.

Badala yake, kwa mujibu wa Dr Meave Leakey wa chuo cha Turkana Basin mjini Nairobi, aliyeongoza utafiti huo anasema kua uvumbuzi huu tofauti ilikuepo mapema katika kubadilika kwetu kama viumbe.

Dr.Leakey ameiambia BBC kuwa kama viumbe tumepitia mabadiliko kwa njiia moja na wanyama wengine walivyobadilika. Hatukua na tofauti yoyote hadi tulipoanza kuunda vifaa vya mawe''

Katika aina nyingine za wanyama, kila mmoja amepitia mabadiliko mbalimbali, kila moja wao na aina mpya ya tabia maumbile, kama mabawa, au miguu yenye kucha zisizo baini kucha. Ikiwa aina mpya ya maumbile haikidhi mahitaji na kuendana na mazingira basi kiumbe mpya ataendelea kuishi vinginevyo anatoweka kabisa.

Kwa mujibu wa Profesa Chris Stringer wa jumba la kumbukumbu au Natural History Museum mjini London, ushahidi wa visukuku na mafuvu unazidi kuonyesha kua mabadiliko ya viumbe yalifuata mkondo mmoja.