Mazishi ya Meles Zenawi kwa picha

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 15:44 GMT

Mazishi ya Zenawi kwa picha huko Addis

  • Jeneza la Marehemu Meles Zenawi lilifika katika uwanja huu mjini Addisa Ababa kwa mazishi ya kwanza ya kitaifa katika kipindi cha miaka sabini
  • Jeneza la hayati Zenawi lilikuwa hapa kwa watu waliofika kutoa heshima zao za mwisho
  • Baadhi ya wananchi walijawa na majonzi wakati wakimpa mkono wa buriani hayati Zenawi
  • Mama huyu hangeweza bila shaka kuzuia majonzi wakati waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Meles.
  • Maelfu ya waombolezaji walifika katika uwanja huu ambako mabango ya hayati Zenawi yalikuwa kila mahali konyesha watu hapa walivyokuwa wanamuenzi
  • Picha za zenawi zilikuwa katika kila sehemu ya mji wa Addis Ababa
  • Bango hili ni ishara kuwa Meles alikuwa kipenzi cha wengi nchini Ethiopia
  • Na wanajeshi hawa hawangeweza kujizuia kwa majonzi
  • Bendera za Ethiopia zilikuwa kila mahali kuonyesha uzalendo kwa nchi na hayati Zenawi alivyowaleta pamoja watu wa tabaka mbali mbali.
  • Meles alipendwa na wote nchini Ethiopia kama mwombolezaji huyu aliyevalia T shirt yenye maneno ya kumuenzi Zenawi

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.