Wachimba migodi wa Marikana wazikwa

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 10:13 GMT

waomboleza marikana

  • Maelfu ya waombolezaji nchini Afrika Kusini walihudhuria misa ya wafu katika mgodi wa Marikana ambako wachimba migodi 34 waliokuwa wanagoma waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa mgomo wao
  • Picha za huzuni na majonzi zilikuwa wazi wakati wa misa hiyo
  • Wafanyakazi wa jamii waliombwa kuwashughulikia waombolezaji waliohitaji kusaidiwa
  • Baadhi ya jamaa za waliofariki walizirai baada ya kushindwa kukabili hisia zao
  • Waombolezaji waliimba nyimbo za kumsifu Mungu katika lugha za Xhosa na Zulu katika mahema makubwa yaliyowekwa katika eneo la mauaji
  • Viongozi wa kanisa kutoka madhehebu mbali mbali pamoja na wanasiasa walijiunga na maelfu ya waombolezaji kutoa pole zao.
  • Nje ya mahema, mamia ya wachimba migodi, walisikiza hotuba wakiwa katika kilima kinachojulikana kama "Hill of Horror" ambako mauaji yalifanyika.
  • Viongozi wa dini, waliongoza maombi na kuwataka watu kutolipiza kisasi kwa kile kilichotokea.
  • Wakati waombolezaji wakikusanyika, rais Jacob Zuma alitangaza maelezo ya tume itakayochunguza mauaji hayo. Alisema tume hiyo itakamilisha uchunguzi wake katika miezi michache ijayo

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.