Wizi wa chokoleti Bukini

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 17:52 GMT
Kakao

Wizi wa zao la kakao lawaudhi wakulima wa Madagascar

Ni usiku eneo la kaskazini-magharibi mwa Bukini (Madagascar), hofu zimetanda juu ya nyuso za wafanyakazi wa mashambani wakati wanapokutana katika kijiji chao, Antanimandririna, kujadili mgogoro: Jinsi ya kulinda zao tamu duniani linalopendwa zaidi na raia wa nchi za Magharibi ambalo limekuwa likiporwa na majambazi wenye silaha.

Amory, mwenye umri wa miaka 62 anaelezea kiwango cha uhalifu huo.

"Sisi tulikuwa tumehifadhi mavuno yetu ya hivi karibuni katika maghala makubwa ya mbao nyuma ya nyumba, wakati tulipoamka tukakuta mazao yote yameibiwa," anasema.

"Watu walifika na bunduki na kuwatishia wakulima - watokea msituni na tumesikia tukio jingine katika vijiji vya jirani kwamba mazao yao pia yameibiwa."

Madagascar ni chanzo kikubwa duniani cha kokoa nyekundu inayotengeza chocolate nzuri inayotumika leo Ulaya na Marekani .

Mbegu hizo za kakao ambazo hutumika kutengeneza chocolate ya kiwango cha juu mwanzo hazikuwa na mahitaji makubwa sana.

Kuongezeka ladha na utamu wa chocolate ambayo chanzo ni kwa mzalishaji mkulima imelifanya zao hilo sawa na dhahabu nyeusi"

Kuendelea kupendwa kwa chocolate kumeongezeka bei ya baadhi ya aina ya kakao katika miaka michache iliyopita, ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakinunua mbegu bora ya kakao kwa bei mara 10 ya bei ya kakao duniani.

'Kichaka wa wahalifu'

Kwa wakulima wa kisiwa maarufu kwa zao la kakao, mahitaji ya chocolate dunia ni lazima yalete mabadiliko kwa wakulima kutoka katika maisha ya umaskini, lakini maisha yao mapya yanatishiwa na majambazi yenye silaha wanayozidi kuenea katika maeneo ya vijijini, wanaoteka maghala na magari yanayosafirisha mbegu za thamani ambazo zinatengeza chocolate.

Katika baadhi ya vijiji, majambazi wameiba kokoa yenye thamani ya karibu dola za marekeni 1,000 (sawa na paundi za Uingereza 630) katika moja ya nchi maskini zaidi duniani.

" Tunateseka hapa. Kakao yetu ni miongoni zao bora lakini hatuwezi kuilinda. Majambazi yanatokea msituni na kuiba" mkulima mwingine, Floren, anasema .

Hakuna polisi mahali popote. Hii ni sehemu ya wahalifu na wanaweza kufanya chochote wanachotaka na wametuacha pasipo njia ya kulisha watoto wetu. Wanaweza kuwa ni watu maskini lakini wao wanawaibia watu maskini zaidi. " alisema.

Katika kisiwa hicho, umaskini ni jambo linalozungumzwa.

Vikwazo vya kimataifa vya kiuchumi vilivyowekwa kwa Madagaska baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomweka Rais Andry Rajoelina madarakani mwaka 2009, umefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Bei kubwa ya chakula, na magonjwa kama vile malaria na majanga mengine yamelizinga taifa hilo.

Kwa wakulima kama Amory, mgogoro wa kisiasa na kiuchumi ulioshika moyo wa kisiwa hicho imeacha watu wanoishi maeneo ya kijijini kusubiri huruma ya watu wenye silaha.

Leo hii, kulingana na Utafiti wa shirika la Silaha Ndogo Ndogo la Yearbook, theluthi moja ya Madagascar imekuwa (Kanda nyekundu), kufuatia serikali kutoa ulinzi kidogo au mahali pengine kutokuwa na udhibiti kwa majambazi au wezi.

Katika baadhi ya maeneo ukosefu polisi umesababisha wanakijiji kuchukua sheria mkononi.

Mwezi June mwaka huu, mfululizo wa mapigano makali kati ya majambazi na wakulima kufuatia wizi wa mifugo karibu 900 karibu na kijiji cha Ilambohazo eneo la mkoa wa kusini-mashariki wa Anosy, limefanya vikosi vya usalama vya Madagascar kutumwa katika eneo hilo.

Mbegu za kakao chini ya vitanda

Watu wachache ndani ya serikali wanazungumza kuhusu ujambazi lakini baadhi maafisa wa polisi wandamizi wameonyesha hasira katika ukosefu wa ulinzi kwa ajili ya wakulima wa kakao wanaofanya kazi ngumu.

Akizungumza na BBC kwa masharti ya kutokutajwa, afisa mmoja alisema: "Tuna uwezo mdogo wa kudhibiti maeneo ya vijijini ambapo wahalifu wamekuwa wakifanya uhalifu. Hatuwezi hata silaha za kulinda watu hawa..

" Hatuna hata polisi wa kutosha au magari ya doria na matokeo yake wahalifu wanaendesha mambo yao hapa katika kichaka."

Kwa mujibu wa Yohana Ferry, Mkurugenzi Mtendaji wa Madecasse, kampuni pekee ya kimataifa yenye kiwanda kinachotengeza chocolate katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, amesema kakao inapaswa kulindwa kwa sababu inaweza kuwa sekta kutoa ajira.

"Wakulima wa kakao hawapewi ulinzi. Ni ajabu wewe fikiria tani ya kakao yenye thamani kama $ 6,000 (£ 4,000) unaweza kuchota " Ferry alisema.

"Hiyo imebadilisha maisha ya watu na kufanya watu wajaribiwe kufanya wizi wa kutumia silaha. Wakati mkulima anateseka, wafanyabiasha wetu wanateseka sana -. Tunategemea mzunguko wa kokoa.

Madagascar lazima ijilinde kama nchi inayoongoza kama muuzaji mkubwa wa vanilla nje.

Kwa kiasi kikubwa zao la vanilla duniani linatoka katika kisiwa hicho na maganda yake yamekubwa yakidhibitiwa.

Hauwezi kusafirishwa usiku na adhabu kwa kuiba zao hilo ni kali.

"tunadhani kakao nayo ipewe ulinzi kama huo," Ferry alisema.

Mashamba mengi makubwa wameajiri walinzi wenyewe wenye silaha kulinda maghala ya kakao lakini wengi ya wakulima hawana uwezo huo zaidi ya kuficha mbegu za kakao katika nyumba zao wenyewe, na hata chini ya vitanda ambapo watoto wao hulala.

Amory ni mmoja wa wakulima wengi ambaye sasa anafikiria kununua bunduki ili kulinda maisha yake akiwa kijijini.

"tunageuka kuwa silaha sisi wenyewe na hii itafika mwisho lini?" aliuliza.

"Sisi ni wakulima. Hatupaswi kubeba silaha ili tuweze kuishi."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.