Makala ya Sema Kenya kuzinduliwa

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 15:36 GMT

Washiriki wa Sema Kenya

Shirika la BBC likishirikiana na kituo cha televisheni cha NTV nchini Kenya, zinapanga kuzindua kipindi kipya kiitwacho, Sema Kenya.

Uzinduzi wa kipindi hicho utakuwa Septemba 30, 2012.

Kipindi hicho kitatoa fursa kwa wakenya kuuliza maswali nyeti wanayokabiliana nayo na viongozi watawajibishwa kuyajibu maswali yao.

Sema Kenya ambacho ni kipindi cha mjadala, kitajumuisha wakenya wa tabaka mbali mbali na jopo la viongozi.

Katika kipindi cha miezi sita ijayo, kipindi hichi kitazuru maeneo tofauti ya nchi kukutana na wakenya wa tabaka mbali mbali.

Msimulizi wa Sema Kenya ni mwandishi mashuhuri Joseph Warungu, ambaye wakati mmoja alikuwa mhariri wa Afrika wa BBC.

Kipindi hichi zaidi kitaangazia maswala ya demokrasia na utawala bora huko wakenya wakijiandaa kupiga kura yao Machi , 2013.

Sema Kenya kitapeperushwa kila Jumapili kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC na runinga ya NTV nchini Kenya. Makala haya pia yatasikika kupitia vituo vingine vitano vya redio na kupitia wavuti wa BBC Swahili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.