Hasira katika nchi za kiarabu

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 13:16 GMT

Maandamano katika nchi za kiisilamu.

 • Hapa bendera ya Marekani iliteketezwa ishara ya hasira waliyokuwa nayo waumini wa dini ya kiisilamu
 • Maandamano yalifanyika katika nchi za kiarabu kama vile Misri, Tunisia, Morocco, Yemen na kwingineko
 • Ghasia zilianzia nchini Libya katika mji wa Benghazi ambako ubalozi wa Marekani uliteketezwa
 • Huu ni ubalozi wa Marekani nchini Libya uliovamiwa baada ya filamu hiyo kuwafikia waisilamu chini humo.Ghasia hizo zilisababisha kifo cha balozi wa Marekani na maafisa wengine wanne wa ubalozi huo.
 • Maelfu ya waisilamu walijitokeza kuonyesha kero lao kuhusu filamu hiyo
 • Na nchini Libya bendera ya Marekani ilikuwa matatani hapa ikiraruliwa na kwingineko ikiteketezwa
 • Polisi wa kupambana na ghasia walikuwa na wakati mgumu kudhibiti maandamano ya mamia ya waisilamu kote duniani
 • Waisilamu walijitokeza kumtetea mtume Muhammad na kupigania sifa yake kinyume na ilivyoonekana katika filamu iliyochochea hisia kali miongoni mwao
 • Fujo na ghasia zilizokumba mataifa ya kiarabu waisilamu wakipinga filamu -Innocence of Muslims-
 • Waisilamu kutoka mataifa ya kirabu Kaskazini mwa Afrika walionyesha umoja wao katika Uisimalu na kulaani filamu hiyo
 • Ubalozi wa Marekani nchini Libya ukiteketea
 • Hapa ni makundi ya vijana wa kiisilamu waliojitokeza kufanya fujo kama ishara ya kero zao kuhusiana na filamu iliyotolewa huko nchini Marekani
 • Mabango yalibebwa yakiwa na maandiko ya sifa ya Mtume Muhammad kukashifu taswira iliyotolewa kuhusu Mtume kwenye filamu hiyo

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.