Ghasia za Tana River kwa picha

Imebadilishwa: 17 Septemba, 2012 - Saa 17:25 GMT

Picha za Tana

 • Tangu kuanza kwa ghasia, serikali ya Kenya imepeleka polisi wa kupambana na ghasia ingawa wanasiasa wa eneo la Tana River walisema kuwa polisi walionekana kushindwa na kazi yao ya ulinzi
 • Waathiriwa wa ghasia hizo walikuwa wengi kuanzia kwa watoto na watu wazima. Jamii za Pokomo na Orma zilishambuliana zikiwa zimejihami kwa mapanga na mishale huku wengine wakiwa wamejihami kwa mishale na bunduki
 • Mama huyu alikuwa mmoja wa wale walioathirika na kujeruhiwa vibaya
 • Damu ilikuwa imetapakaa kwenye kuta ishara ya mauaji yaliyofanyika wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe
 • Watoto walikuwa miongoni mwa walioathirika kutokana na vita hivyo na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu
 • Chakula kilichokuwa kimehifadhiwa kwa maghala pia kiliteketezwa
 • Nyumba ziliteketezwa
 • Nyingine zikibomolewa na kuvunjwa vunjwa
 • Hasara iliyotokana na mashambulizi huku nyumba zikiteketezwa
 • Watu walilazimika kukimbilia usalama wao na kuacha mali zao
 • Mifugo nao hawakusalia
 • Hawa ni miongoni mwa watu waliolazimika kukimbilia usalama wao na kwenda katika kambi za muda
 • Waathiriwa wa vita kambini

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.