Mwongozo Kwa Wapiga Kura

Imebadilishwa: 21 Septemba, 2012 - Saa 06:54 GMT

Sehemu hii inakusudiwa kuwa mwongozo wa raia katika kupiga kura.

Uchaguzi Kenya hufanyika baada ya kila miaka tano. Uchaguzi mkuu ujao unatarajiwa kufanyika 4 Machi mwakani kwa mujibu wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC).

Wapiga kura watapiga kura katika ngazi tofauti kuchagua viongozi wa Serikali ya Kitaifa na Serikali za Kaunti.

Tume huru ya uchaguzi itaanza usajili rasmi wa wapiga kura kutoka tarehe 30 Oktoba hadi mwisho wa mwezi huo.

IEBC ndio itakayotoa ratiba ya uchaguzi na pia ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa vyama vya kisiasa kwa uchaguzi mkuu ujao.

Nyadhifa zitakazogombewa katika uchaguzi 2013

Mtu mmoja apiga kura yake

Kwa mujibu wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, kuna nyadhifa sita ambazo zitagombewa katika uchaguzi mkuu zikiwemo:

Rais

Mbunge

Seneta

Gavana

Mwakilishi wa wanawake

Mwakilishi wa Serikali ya Kaunti

Rais

1. Kuchaguliwa kwa Rais.

Rais atachaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi waliosajiliwa katika uchaguzi mkuu. Ili kuchaguliwa, mgombeaji lazima apate angalau kura asilimia hamsini na kura moja kutoka kura zote zilizopigwa na pia apate angalau asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa angalau katika kaunti ishirini na nne (24).

2. Iwapo hakuna mgombeaji atakayepata angalua kura asilimia hamsini na kura moja ya kura zilizopigwa na angalau asilimia ishirini na tano katika kaunti ishirini na nne, wangombeaji wawili walio na kura nyingi zaidi watashindana tena katika uchaguzi mpya.
3. Uchaguzi mpya lazima ufanyike katika kipindi cha siku thelathini baada ya awamu ya kwanza ya uchaguzi.
4. Mgombeaji ambaye atapata idadi kubwa zaidi ya kura kwenye uchaguzi mpya atatangazwa kuwa Rais.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.