Sikati tamaa! mikahawa ndiyo biashara yangu

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 09:51 GMT

Ahmed Jama kwenye mkahawa wake

Ahmed Jama ana mkahawa mwingine katika ufuo wa bahari mjini Mogadishu.

Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga mjini Mogadishu walilenga mkahawa mmoja maarufu mjini Mogadishu siku ya Alhamisi wiki iliyopita saa za jioni na kuwaua watu 14

Ahmed Jama, mmiliki wa mkahawa wa 'village Restaurant' alirejea nyumbani Mogadushu miaka minne iliyopita kutoka nchini Uingereza kwa lengo la kuanza biashara.

Yeye ni mmoja wa raia wengi wa Somali walioamua kurejea nyumbani kusadia katika juhudi za kuikarabati nchi yao iliyozongwa na vita

Aliambia BBC kuhusu shambulizi hilo, uamuzi wake wa kurejea nyumbani na matumaini yake kuhusu mustakabali wa Somalia.

''Yaani siwezi kuamini mambo ambayo yametokea.

Siwezi kulia lakini nahisi uchungu.

"Nahisi kama viongozi wameniangusha"

Najisikitikia sana na kuwahurumia wafanyakazi wenzangu pamoja na marafiki zangu waliouawa kwenye mlipuko huo.

Shambulio lilitokea saa kumi na mbili jioni zikiwa zimekatika dakika 10 kabla tu ya sala ya Magharibi.

Mmoja wa ashambuliaji wa kujitoa mhanga alikuwa ndani ya mkahawa akiwa amevalia vesti, na mwenzake akiwa na bunduki. Alimpiga risasi muosha magari aliyekuwa nje. Kisha baadaye mwenzake aliyekuwa ndani akajilipua.

Nje kila mtu alikuwa anajaribu kukimbilia usalama wake , akimtoroka mshambuliaji aliyekuwa amejihami wakawa wameingia ndani ya jengo lililokuwa karibu. Wakati huo Yule mshambuliaji wa pili naye akajilipua kwa guruneti.

Zaidi ya watu kumi na tano waliuawa, na wengine wengi wakajeruhiwa. Hili sio jambo la kawaida.

Lakini nahisi kama viongozi hawanijali. Nahisi kama hao wanasiasa wanajijali wenyewe. Wana ubinafsi mwingi.
Mimi naajiri zaidi ya wafanyakazi 100 katika mikahawa mitatu, hasa mjini Mogadishu. Nina mkahawa mwingine mmoja mjini London.

Waliouawa kwenye shambulizi hilo walizikikwa siku ya Ijumaa

Mkahawa ulioshambuliwa uko katikati mwa Mogadishi karibu na ukumbi wa maonyesho.

Mkahawa mwingine ulioko karibu na bahari na ambao namiliki, mimi mwenyewe nina mikakati ya kuweka usalama. Nina walinzi wangu ambao hukagua watu wanaoingia humo na kutoka nje.

Lakini kwa huu ulioshambuliwa, kwa sababu ya eneo ambapo uko, sikuruhusiwa kuwa na mkakati wangu binafsi wa usalama.

Niliwauliza polisi na meya wa mji kwa nini siruhusiwi kuwa na usalama wangu. Nilitaka kupewa mlinzi lakini sikupata jibu.

Waliniarifu kuwa kuna polisi katika eneo hilo kwa sababu wanakarabati nyumba iliyoko juu ya mkahawa. Lakini hawakunisikiza niliposema kuwa usalama wao hautoshi.''

'KUREJEA NYUMBANI'

''Nilirijea Mogadishu mwaka 2008. Nilikuwa nimeishi Uingereza tangu mwaka 1989. Mojawapo ya maeneo niliyoishi nikiwa Uingereza ni katika mtaa wa Birmingham - huko ndiko nilisomea

Nilisomea somo la upishi kabla ya kuwa mpishi mwenyewe. Nilifanya kazi Birmingham kabla ya kuhamia mjini London nikinuia kupata uzoefu zaidi wa kazi yangu ya upishi na kisha nikafungua mikahawa yangu.

Niliamua kurejea nyumbani angalau kujaribu kukwamua nchi yangu

Nilikuwa najaribu kuwashawishi waekezaji wengine kama mimi kwamba ikiwa naweza kurejea mwenyewe kwanza na nifanikiwe, basi na wao wanaweza kuja.

Ahmed Jama alisema kuwa alikuwa ameomba usalama zaidi

Familia yangu ingali inaishi London. Mke wangu anasimamia mkahawa wangu mmoja unaojulikana kama 'the Village' , wanangu wako huko pia.

'Nitafungua mkahawa huo kwa mara nyingine - nitajaribu wala sitachoka.

Familia yangu inanishawishi niweze kurejea London. Hawataki niendelee kuishi japa.

Lakini , mimi ndiye nilianza biashara hii na nataka niikamilishe . Haya ndio maisha yangu.

Huenda nikawa mmoja wa watu watakaokumbukwa na wala sitaki kuishi bila maono yangu.

Nitaufungua tena mkahawa huo - nitajaribu na wala sitakataa tamaa.

Uamuzi wangu ni kufanya kazi na wakati bado nikiwa hai, nitaendelea. Mimi ni mfanya biashara mwenye mikahawa mingi na sina budi ila kuendelea na kazi hiyo.''

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.