Unakumbuka Tintin? tembea DRC

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 12:03 GMT

Hekaya za Tin Tin DRC

  • Huku mji wa Kinshasa ukijiandaa kwa mkutano wa nchi za kifaransa wakati maelfu ya wageni kutoka nchi hizo watamiminika katika mji huo mkuu wa DRC , watengeza sanamu mjini humo tayari wameanza kutayarisha masoko yao wakianza kwa sanamu za kumbukumbu ya kipindi maarufu cha Tintin. Nchi hiyo ilikuwa na mashabiki wengi wa kitabu maarufu cha - Tintin in the Congo kilichoandikwa na mwandishi maarufu wa Ubelgiji Herge.
  • Hata hivyo, kitabu hicho kilichoandikwa mwaka 1931, sasa kimeibua utata kwa sababu ya kugusia hisia za kibaguzi. Mapema mwaka huu, mahakama nchini Ubelgiji, ilikataa ombi la kupiga marufuku kichwa cha kitabu hicho kwa madai ya kukiuka sheria za ubaguzi wa rangi.
  • Auguy Kakese mtengeza sanamu, amekuwa akijikimu kimaisha kwa kutengeneza maelfu ya sanamu za Tintin akiwauzia watalii, haoni ubaya wowote kuhusu kitabu hicho. ''ni kichekesho tu, sio ubaguzi wa rangi, kwa wale wanaosema ni ubaguzi wa rangi, nasema kwamba katika uandishi wa vichekeso, hakuna picha zake zozote akionekana kumuua mkongomani, aliambia shirika la habari la Reuters.
  • Kitabu hicho kinasimulia visa vya kijana mdogo katika heka heka zake maishani katika nchi hiyo ambayo ni koloni ya zamani ya Ubelgiji, na inajumuisha visa vya kijana huyo kukutana na walanguzi wa almasi na wawindaji wa wanyama pori.Herge ambaye jina lake la kweli ni George Remi - baadaye alikubali kwamba baadhi ya sehemu za kitabu chake zinaleta aibu. Sehemu moja ya kitabu hicho ambapo Tintin alikuwa anatoa mafunzo ya jiografia, baadale ilibadilishwa ikawa funzo la hesabu.
  • ''Tulikuwa koloni ya Ubelgiji-lakini kwa sababu tunajihusisha sana na Tintin sio kusema kuwa wabelgiji bado ni ndugu zetu.'' Bwana Kakese aliyasema hayo katika karakana yake ya kutengezea sanamu zake,ambako anawajiri wafanyakazi 10 ambao hutengeza sanamu kutoka kwa mbao. Tintin huandamana na mbwa wake mweupe ajulikanaye kama Snowy na rafiki yake ajulikanaye kama Captain Haddock. Waigizaji wengine ni mwanasayansi Cuthbert Calculus, na majasusi Thomson na Thompson pamoja na mwimbaji wa opera Bianca Castafiore.
  • Maelfu ya sanamu za Tintin hutengezwa katika karakana hii na kupakwa rangi hapa. Nyingi ya sanamu hizo ni picha za vitu kutoka Ulaya lakini bwana Kasese haogopi kutengeza sanamu za kiafrika.
  • ''Tintin ni sanamu inayoleta taswira ya picha za kimagharibi na inaonyesha wazi kuwa watu hawa haelewi jamii yatu na tamaduni zetu,'' Joseph Ibongo Gilungule, afisaa mkuu mtendaji wa jumba la kitaifa la makumbusho mjini Kinshasa aliambia shirika la Reuters . Anawataka wakongomani kugusia mambo yanayohusu nchi yao. Lakini ukitafakari kuhusu hilo, sanamu za Tintin hapa zinauzwa kwa kati ya dola 15 na 1,500 , basi bwana Ibongo atakuwa na wakati mgumu kuwashawishi wachuuzi wa Kinshasa kuiacha kazi hii.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.