Makala mapya ya Sema Kenya

Imebadilishwa: 25 Septemba, 2012 - Saa 12:01 GMT

Kipindi Sema Kenya kwa picha

 • Jopo la Sema Kenya

  SemaKenya ni makala mapya ya mjadala wa kisiasa yanayoandaliwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC na kusambazwa kila wiki kwenye TV, redio, na kwa mtandao wa tovuti nchiniKenya.

 • Msimulizi Joseph Warungu

  Joseph Warungu ndiye mtangazaji na mwendesha mjadala wa kipindi cha Sema Kenya. Warungu ni mwandishi mashuhuri ambaye alikuwa mhariri wa Idhaa ya Afrika ya Kiingereza ya BBC kwa miaka mingi.

 • Mwanajopo Sofia Abdi

  Wakati WaKenya wanapojiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa 2013, kipindi cha SemaKenyakitazuru kote nchini kujumuisha watu ili watoe masuala ya eneo zao nay a kitaifa kwa jumla.

 • Washiriki

  SemaKenyani kipindi maalum ambapo hoja zitaamuliwa na washiriki wala sio msimulizi.

 • Mwanamke mshiriki

  Kipindi cha SemaKenya kitajumuisha watu wa tabaka mbalimbali wakiwemo wanaume, wanawake na vijana.Mwananchi wa kawaida atapata fursa ya kuwahoji viongozi ana kwa ana.

 • Washiriki

  Kitafanyiwa kwa lugha ya taifa ya Kiswahili.Hoja zinazozungumziwa zimetokana na utafiti wa kuonyesha masuala yanayohusu eneo tunazotembelea.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.