Sema Kenya - Jukwaa la Wakenya

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 07:25 GMT

Kikao cha Kajiado

Sema Kenya…jukwaa la WaKenya wote, jiunge na mjadala wa kitaifa.
Sema Kenya ni kipindi cha mjadala, cha muda wa saa moja, ambacho hupeperushwa kupitia redio, televisheni na kwenye tovuti.

Kipindi hiki kinazuru maeneo tofauti ya nchi, huku Wakenya wakijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka ujao. Lengo ni kuwapa wananchi fursa ya kuelezea hoja zao, kupata taarifa na kushiriki katika mjadala wa kitaifa.

Tangu kilipozinduliwa mwezi Oktoba, Kipindi cha Sema Kenya kimefaulu kuandaa mijadala mikali iliojumuisha wananchi ikiangazia masuala ya usalama, mihadarati, ukabila, ugatuzi, ugavi wa ardhi na marekebisho ya sheria za ugavi wa ardhi.

Mada za kila kipindi huamuliwa na washiriki.

Watu wanaweza kushiriki katika mazungumzo haya ya kitaifa kupitia tovuti ya BBC, mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Aidha njia nyingine Sema Kenya inawafikia wananchi ni kupitia mashirika ya kijamii ambayo kipindi hiki kinashirikiana nao.
Mtindo wa Sema Kenya:
• Lugha: Sema Kenya inaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili.
• Utafiti: Sema Kenya inategemea utafiti wa kina kufanikisha makala haya.
• Wanaoshiriki: Kinahusisha watu wa tabaka mbalimbali; vijana kwa wazee, wanawake na wawakilishi wa vikundi maalum.
• Huwaleta pamoja wananchi na viongozi wao: Wananchi wa kawaida na jamii zilizotengwa wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao.
• Mada ya mjadala huamuliwa na washiriki katika kipindi hiki.
• Haibagui, haipendelei na inashirikisha kila moja kupitia redio, televisheni na kwenye tovuti.
• Mjadala huendelea kwenye mtandao wakati kipindi kikiwa hewani hata baada ya kutia tamati kwenye redio na televisheni.
Tazama, Sikiliza na ushiriki kwa Sema Kenya
Televisheni: KTN, kila Jumapili saa 6 jioni.
Redio: Idhaa ya Dunia ya BBC (Nairobi 93.9FM, Mombasa 88.1FM) na kupitia kituo cha Pamoja FM kila Jumapili saa saba alasiri.
Mtandao: bbcswahili.com/semakenya
Facebook: BBCSemaKenya
Twitter: @ bbcsemakenya
Sema Kenya ... Jukwaa la Wakenya, jiunge na mazungumzo ya kitaifa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.