Afrika kwa picha

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 15:29 GMT

Afrika wiki hii barani Afrika

  • Huu ni mchezo wa Rodio uliofanyika nchini Afrika Kusini, viungani mwa mji wa Cape Town. Ndiyo mchezo wa pili wa aina hii kufanyika katika mkoa wa Western Cape na hapa wachezaji huzingatia sheria na kanuni za mchezo huu nchini Marekani.
  • Nchini Nigeria, mtaa wa mabanda wa Makoko, ambao unaelea kwenye maji taka, unatarajiwa kubomolewa na maafisa wa utawala wa mitaa. Huyu msichana mdogo ambaye alikuwa anaendesha mtumbwi wake kwenye maji siku ya Alhamisi.
  • Hawa ni wanawake nchini Afrika Kusini waliovalia mavazi ya kitamaduni ambayo huvaliwa na watu wa kabila la Zulu kusherehekea siku ya turathi nchini humo . Hapa wako kwenye barabara za mji wa Durban pwani mwa nchi hiyo.
  • Maadhimisho ya miaka kumi ya ajali ya feryy ya Joola nchini Senegal, mke na mumewe hapa wametembelea makaburi ya watu waliofariki katika ajali hiyo. Haya ni takriban makaburi 140 ya waathiriwa. Wengi wa watu 1,863, waliofariki katika mojawapo ya ajali mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo walikuwa watoto.
  • Takriban wanachama 200 wa Al-Shabab wanaelekezwa katika mji mkuu Mogadishu baada ya kujisalimisha kwa majeshi ya AU Mogadishu,mwishoni mwa wiki.
  • Huyu ni mmoja wa maharamia walio katika ufuo wa Somalia akiwa amejifunika uso wake. Anasimama karibu na meli ya Ufilipino ambayo iliwahi kutekwa ingawa wafanyakazi wake waliachiliwa baada ya wamiliki kulipa kikombozi.
  • Magari hapa yanajaribu kuvuka mto Niger ambao ulifurika karibu na eneo la Lokoja katika jimbo la Kogi nchini Nigeria
  • Siku moja kabla ya Sudan na Sudan Kusini kutia saini makubaliano kuhusu biashara kati yao,mafuta na usalama na hivyo kumaliza hali ya wasiwasi ambayo nusura itumbukize nchi hiyo kwenye vita, hapa mvuvi anaonekana kwenye mtumbwi wake Sudan Kusini karibu na mpaka mjini Malakal kwenye mto Nile
  • Wanajeshi wa Ivory Coast wanashika doria katika mji wa mpakani wa Noe ambako malori yamezuiwa kuvuka na kuingia nchini Ghana baada ya msururu wa mashambulizi yaliyofanywa nchini Ivory Coast na watu waliokuwa wamejihami . Watu hao walishukiwa kuingia kutoka upande wa Ghana.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.