Ni ubabe dhidi ya maskini duniani?

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 08:19 GMT

Idadi ya watu duniani inaongezeka au kupunguka?

Shirika la umoja wa mataifa la kukadiria idadi ya watu, UNFPA, hivi maajuzi ilichapisha ripoti iliyoangazia hali ya watu kuzeeka duniani.

"Hii leo hali ni kuwa mtu mmoja kwa kila watu tisa ana umri wa miaka 60 au zaidi’’ alisema datari Ann Pawliczko, "lakini ifikapo mwaka 2050, hali itakuwa, kati ya kila watu watato mmoja atakuwa na umri wa miaka 60 na wakati huo kutakuwa na wazee wengi duniani kuliko watu walio chini ya umri wa miaka 15.’’

Umoja wa mataifa unaziona takwimu hizi kama sababu ya kusherehekea kwa sababu watu wanaishi muda mrefu zaidi. Lakini pia una wasiwasi kuwa mabadiliko haya yanaleta changamoto za kiuchumi na kijamii.

Dr Pawliczko angependa kuona nchi zikijiandaa kukabiliana na mabadliko haya kwa sababu hakuna wasiwasi kuwa hali inabadilika.

"Hakuna shaka kuhusu idadi ya watu itakapofika mwaka 2050 kwa sababu wale watakaokuwa na zaidi ya miaka 60 ifikapo mwaka 2050 tayari wamezaliwa. Sio utabiri huu, bali hivyo ndivyo hali itakavyokuwa.’’ Alisema daktari Pawliczko.

Watoto nchini Bangladesh

Hata hivyo kuna taswira nyingine kwa hali hii ya idadi ya watu duniani. Idadi ya watu wanaozaliwa.

Hata hivyo, kutabiri ambavyo hali itabadilika ni vigumu. Kwa mda mrefu watafiti wa idadi ya watu wameona katika takwimu kile wanachokiita hali ya mpito kwa idadi ya watu duniani, kitu kinachojitokeza wakati utajiri unakithiri katika jamii.

"Hali hii ya mpito inajitokeza pia wakati idadi ya vizai vipya na vifo ninapungua katika jamii. Na hili hujitokeza wakati maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanadhihirika.” anasema daktari Pawliczko.

"kwa kawaida tunazungumzia awamu nne katika maendeleo haya. Cha kanza ni idadi ya juu ya vifo na vizazi vipya. Kisha tuna awamu ya pili, kiwango cha juu cha vizazi na kuanguka kwa idadi ya vifo. Kisha tuna awamu ya tatu ambapo idadi ya vizazi inapungua pamoja na kupungua kwa vifo. Na kisha awamu ya nne ambapo idadi ya vizazi na vifo inapungua kwa pamoja , ishara ya idadi ya ukuwaji wa idadi ya watu kupungua.”

Kwa hivyo wakati nchi zinapoendelea kustawi na kutajirika viwango vya uzazi vinashuka. Lakini nini athari yake? Wadadisi wanahofia kuwa nchi tajiri zinasalia katika hali duni ya uzazi.

Lakini utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa huenda dhana hiyo sio sahihi.

"Tukiangalia katika historia, viwango vya uzazi vimekuwa vikianguka barani Ulaya.'' alisema Professa Jane Falkingham, mkurugenzi wa kitivo cha kukadiria idadi ya watu katika chuo kikuu cha Southampton Uingereza.

Watafiti huenda wakachukua muda kuweza kuchanganua hili kwa sababu wazo la kuwa nchi zinakuwa tajiri wakati zikiendelea kupata watoto wachache, ni jambo la kushangaza kwao.

Uganda ni mojawapo ya nchi ambazo idadi ya watu wake imeongezeka kupindukia

Huku idadi ya watu ikiongezeka na kukaribia watu bilioni saba, kinachohojiwa ni ikiwa juhudi za kudhibiti idadi ya watu zimekuwa kama wakosoaji wanavyosema ubabe dhidi ya watu maskini duniani

Kwa watu bilioni saba, hebu jiulize wewe ni wa ngapi? Swali sasa ni je utafiti huu ulioonyesha kuongezeka kwa kiwango cha uzazi katika nchi zilizostawi unaweza kuonyesha makadirio ya idadi ya watu duniani?

Dr Pawlizcko wa UNFPA anasema kuwa utafiti huu hauwezi kuwa na athari kubwa. Inawezekana yuko sahihi katika tathmini yake. Lakini hakuna mtu aliye na uhakika juu ya swala hili.

Watafiti wamekuwa wakikosolewa kwa kutoweza kutoa utabiri wa uhakika kuhusu mabadiliko katika idadi ya watu duniani.

“Tumekua tukikosea katika kutabiri vilivyo idadi ya watu duniani katika miaka hamsini iliyopita” alisema Professa Falkingham, na kuongeza kuwa sababu ya hili ni dosari katika kutafsiri vyema vigezo vya kuongezeka au kupungua au hata kukuwa kwa idadi ya watu duniani.

Siku moja tutaelewa ikiwa makadario yetu ya idadi ya watu hata baada ya mwaka 2050 ni sahihi, ikiwa kile kinachoitwa kipindi cha mpito katika ongezeko la idadi ya watu duniani , kitaingia awamu ya tano isiyotabirika.

Lakini kutabiri idadi ya watu haiwezi kuwa sayansi yenye uhakika.

Idadi ya watu nchini China

Mnamo mwaka 2004, idara ya kiuchumi na maswala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa, ilijaribu kutabiri idadi ya watu duniani itakavyokuwa mwaka 2300.

Ilisema kuwa idadi ya watu itaweza kudbitiwa itakapofika angalau mwaka 2050 na kisha kusalia katika hali hiyo kwa kipindi hicho kizima. kwa hivyo ina maana kuwa chochote kinaweza kufanyika kuhusiana na mabadiliko katika idadi ya watu duniani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.