Keki ishara ya maisha ya kisasa Ethiopia

Imebadilishwa: 12 Novemba, 2012 - Saa 08:52 GMT

Keki ambazo zimekuwa ishara ya maisha ya kisasa nchini Ethiopia

Ethiopia ni mojawapo ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani afrika licha ya kutokuwa na mafuta, lakini wakati watu wa kipato cha kadri ambao nao wanaongezeka kwa kasi wanataka kuonekana kama ambao wanaishi katika dunia ya kisasa.

Kila unapoangalia kuna viashiria vya maisha hayo mfano kuwepo keki ndogo kama Queen cakes hivi ambazo zimerembwa sana na ambazo zinaenziwa nchini marekani na hata ulaya.

Afrika hii mpya sio ishara ya maisha halisi barani humo.

Keki hizi zinapatikana aina mbali mbali kama vile ,Red Velvet, Caribbean Breeze, Vanilla Fever na Brunette yaani ni nyingi mno.

Nilikuwa nimesimama katika mojawapo ya mikahawa tayari kulipia chakula changu mjini Addis Ababa na nilikuwa nazitimazma keki hizo maarufu kama Cupcakes.

Zikiwa zimepangwa vizuri na kurembwa kwa sukari ya maji maji ambayo hugandishwa.

Rangi ya keki hizo ni ya kuvutia sana. Mkahawa huo ujulikanao kama “The Cupcake Delights Bakery” ulikuwa umejaa pomoni.

Watu waliovalia kupendeza nao wakawa wanakunywa chai kwa keki hizo zenye rangi za kuvutia mno.

Mwanamke mmoja wa kihihindi aliingia kwenye mkahawa huo na kuagiza kupewa keki hizo. Wanaume wachina ambao wanafanya biashara nchini humo hakuwachwa nyuma , pia waliagiza keki hizo kwa wingi.

Upande wa pili wa barabara mkahawa unaojulikana kama The Beer Garden pia ulipendwa sana na Wachina.

Mkahawa huu unamilikiwa na wajerumani ambao hutengeza bia yao wenyewe.

Wafanyakazi wachina wanaonekana wakiwa wamezingira meza moja huku nyuso zao zikaanza kuwa nyekundu , sauti zao zikiwa juu huku wakilewa kweli kweli.

Sababu moja ya mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kubadilika katika miaka mingi iliyopita, ni wachina hawa.

Sawa na maeneo mengine ya Afrika, China iko tayari kupora maliasili ya Afrika huku ikijengea bara hilo barabara, njia za reli na majengo makubwa makubwa.

Kila wakati ninapo zuru Addis Ababa, mimi hujionea majengo makubwa makubwa na bila shaka hunichanganya.

Addis Ababa ni mji wa kisasa ulio katika hali ya utandawazi ingawa ungali na mizizi ya kitamaduni watu wakiishi maisha ya kitamaduni na kupiga siasa.

Wananchi wa Ethiopia wangali na majonzi kufuatia kifo cha Hayati Zenawi

Mji huu ungali katika hali ya simanzi kufuatia kifo cha kiongozi aliyeongoza muda mrefu sana nchi hiyo, Meles Zenawi, ambaye alifariki mwezi agosti.

Hayati Zenawi, ambaye licha ya kuwa mshirika wa karibu wan chi za magharibi, hakuweza kustahimili upinzani, alikuwa na rekodi mbaya ya hak za binadamu, ingawa wancnhi wake hawataki kumuondoa katika nyoyo zao.

Lakini tukiicahana na hayo, turejee katika mada ya Afrika ya kisasa. Baada ya kujionea mchana wenye keki si haba na bia, , nilikumbana na mziki wakati wa jioni.

Mkahawa wa Jazzamba Lounge – ambao ulifungua milango yake miaka michache imepita, sasa, ni ukumbi mkongwe wa densi ambao unasifika kwa kuwa mkongwe zaidi mjini Addis Ababa. Na ni hapa ndipo nilikumbana na eneo lengine ambalo, kwa kweli, tunaweza kusema ni taswira ya enzi ya baada ya utandawazi.

Na niliketi hapa kula pizza, nilitazama watu wakicheza densi aina ya salsa. Muziki kutoka Cuba ulichezwa usiku kucha huku vijana wa Ethiopia nao wakijivinjari.

Nje ya Jazzamba Lounge, hali ilikuwa ya mchakamchaka.

Kwenye kilabu nyengine watu walikuwa wakicheza reggae.

Katika kilabu nyingine nusura nigongane na kahaba mmoja aliyekuwa anachezesha makalio yake karibu na mwanamume mmoja ambaye hakuonekana sana akiwa na hamu naye kwani alikuwa anakunywa bia yake .

Nje ya kibalu kulikuwa na maskini waliokuwa wanaomba pesa

Matumaini na ndoto za watu wenye kipato cha kadri, mjini Addis Ababa' yanasalia kuwa juu.

Ingawa nje kwenye kilabu nyingine nilijionea wanaume wenye asili ya kizungu wakiwa wamewapakata wasichana wadogowadogo ambao wanatosha kuwa watoto wao.

Na asubuhi ilipofika, nipelekwa nyumbani kwa texi nodogo yenye rangi ya buluu na nyeupe ingawa ilikuwa kuu kuu.

Hata saa hii usiku unaweza kuwaona wanawake waliowapakata watoto wao wakiomba omba

Watu waliovalia nguo chakavu wanapanga foleni nje ya majengo ya serikali wakisubiri kitu ambacho kwa kweli hakijulikani kwa sababu ni usiku.

Hii picha ya Afrika mpya niliyojionea mjini Addis Ababa na ambayo pia nimeiona Nairobi, Dakar, Abuja na kwengineko, inafurahisha na yenye matumaini makubwa lakini hiki sio kisa kamili.

Nchini Ethiopia watu wengi wanaishi maisha ya umaskini lakini wana ndoto ya kuwa na maisha mazuri

Ndio! wachina , wasaudi, wahindi wote wanakimbilia hii Afrika.

Ndio kuna idadi kubwa ya watu inayoendelea kukuwa hasa watu wenye kipato cha kadri ambao hununua sana katika maduka ya kifahari, maduka na mikahawa ya Pizza sawa na hali ilivyo Ulaya na Marekani.

Lakini chimba kidogo ndani zaidi, utapata dunia nyingine tofauti.

Kati ya watu milioni 85 na 90 wanaishi nchini Ethiopia , na wengi wao hata hawawezi kuota juu ya keki hizi mbali na kuwa hawana uwezo wa kuchagua wanazotaka katika mkahawa huo nilioutembelea mjini Addis Ababa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.