Sema Kenya kuzuru Makueni

Imebadilishwa: 14 Novemba, 2012 - Saa 14:31 GMT

Mshiriki wa kipindi cha Sema Kenya.

Wiki iliyopita kipindi cha Sema Kenya kilizuru Kaunti ya Makueni iliyoko eneo la Ukambani.

Makueni ni moja ya majimbo matatu Ukambani ikiwa pia na yale Machakos and Kitui.

Kaunti ya Makueni inashirikisha maeneo bunge masita; Makueni, Kibwezi ya Mashariki, Kibwezi ya Magharibi, Kaiti, Kilome na Mbooni.

Kaunti hii hupakana kwa upande mmoja na barabara kuu ya kutoka Nairobi hadi Mombasa.

Baadhi ya miji inayofahamika na wengi katika kaunti hii ni kama vile Kibwezi, Wote, Mtito Andei, Makindu, Mbooni na Emali.

Ni viongozi wengi wa kisiasa kutoka Makueni ambao wameweza kupata sifa ya kitaifa. Kwa mfano Waziri wa Elimu Mutula Kilonzo, Profesa Kivutha Kibwana, aliyekuwa naibu-mwenyekiti wa chama cha DP Agnes Ndetei, kinara wa chama cha PICK John Harun Mwau wote wametoka Makueni.

Mwenyekiti wa chama cha NARC Charity Ngilu pia amezaliwa kaunti ya Makueni.

Masuala yanayoikumba eneo hili ni pamoja na njaa na ukosefu wa maji.

Kwa vile mvua inayonyesha sehemu nyingi za Makueni sio ya kutegemewa, kaunti hii huwa na uchache wa vyakula na ukosefu wa maji.

Mambo haya pia yanachangia kudhuru afya ya wakazi hapo ikikumbukwa kwamba, idadi ya vituo vya afya humo ni duni sana.

Wakazi 100 wa Makueni na jopo la viongozi na wataalamu walikutana kwenye kipindi cha Sema Kenya kushiriki kwenye mjadala wa masuala ya kaunti hiyo.

Makala haya hupeperushwa kupitia redio ya BBC saa saba mchana na kupitia runinga ya KTN nchini Kenya saa kumi na mbili jioni. Pia utaweza kuyapata kupitia vituo vya redio vya Star FM (105.9 Nairobi, Kaskazini Mashariki) na KU FM (99.9 Nairobi) kila Jumatatu saa tano asubuhi na saa 6 jioni mtawaliwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.