Mjadala wa usalama nchini

Imebadilishwa: 29 Novemba, 2012 - Saa 15:00 GMT

Msimulizi wa kipindi Joseph Warungu


Mwaka huu, zaidi ya watu 1000 wameuwawa katika visa vya vurugu, wizi na ugaidi nchini Kenya.

Idadi hii ya maafa ni sawa na ile iliyoshuhudiwa wakati wa vurugu zilizofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

La kusikitisha ni kwamba hata maafisa wa usalama wapitao 100 wamekufa katika visa hivi.

Juzi, maafisa 42 wa usalama waliuwawa na wezi wa mifugo eneo la Baragoi kwa kushambuliwa na kumiminiwa risasi walipokwenda kusaka mifugo iliyoibiwa na kuelekezwa Bonde la Suguta.

Mjini Garissa, wanajeshi 3 waliuwawa kwa kufiatuliwa risasi walipokuwa kando ya barabara.

Visa kama hivi vimeshuhudiwa Wilaya ya Tana, Mombasa, Kilifi na jijini Nairobi.

Mara kwa mara raia wamezua rabsha na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kuwaua watu.

Hofu sasa ni kwamba maafisa wa polisi wameshindwa kuimarisha usalama nchini Kenya.

Sema Kenya iliandaa kipindi maalum cha kuangazia suala la usalama ili kuwapa raia fursa ya kuwahoji viongozi wao.

Kipindi hiki kilitayarishiwa Kaunti ya Nairobi na kuonyeshwa kupitia televisheni ya KTN tarehe 2 Disemba mwaka wa 2012.

Washiriki 100 na jopo la viongozi na wataalamu walijumuishwa katika kikao kimoja Nairobi kujaribu kutatua suala la usalama.

Tazama yaliyojiri katika kipindi kwenye tovuti yetu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.