Wanaume wapambe wa Korea Kusini

Imebadilishwa: 5 Disemba, 2012 - Saa 08:06 GMT

Wanaume nchini Korea Kusini, wana sifa za kipekee. Wanapenda vileo, hufanya kazi kwa nguvu na pia watafanya lolote kupigania nchi yao.

Lakini sasa kampuni kubwa za bidhaa za urembo, zinajionea sifa moja iliyokuwa imefichika kuhusu wanaume hawa. Hamu yao ya kutumia bidhaa za urembo , wanapenda vipodozi ikiwemo poda ya kujipaka uso.

Miaka miwili ya kuwa jeshini ambalo ni sharti kwa kila mwanaume nchini Korea Kusini, kumewaacha wanaume hao wakiwa wamenaswa katika dhana ya jamii kuhusu wanaume , mojawapo ya lalama za wanawake siku hizi.

Kwa hivyo kasumba hii mpya ya wanaume kuenzi vipodozi imewashangaza wengi sana.

Lichja ya matatizo ya kiuchumi yanayokumba dunia nzima, soko la bidhaa za kujipodoa za wanaume nchini Korea Kusini, ilikuwa kwa asilimia kumi ,mwaka jana, kulingana na kampuni ya utafiti wa biashara, Euromonitor International.

Kampuni kubwa ya vipodozi nchini humo, Amore Pacific, inakadiria kuwa soko limekuwa zaidi kwa asilimia kumi na nne na kusema kuwa soko la bidhaa hizo sasa ni la thamani ya dola milioni miatisa.

Yu-jin,mwanafunzi mwenye umri wa miaka 26, hutumia poda maalum ijulikanayo kama BB, kuremba uso wake kila siku, pamoja na bidhaa zingine tano ikiwemo,cleanser, mafuta ya kuzuia athari za uzee kwenye sura pamoja na mafuta yanayotumiwa kwenye macho.

"zamani nilikuwa na vidonda usoni mwangu, lakini nilipoanza kutumia mafuta ya BB, ngozi yangu ilianza kunyoka na sasa watu wananiambia kuwa nimeanza kupendeza sana’’ alisema Yu-jin

Mafuta ya BB zamani yalikuwa yakitumiwa kwa upasuaji wa kubadilisha umbo la watu….au (plastic surgery) ili kuficha makovu ya upasuaji ule baada ya matibabu. Lakini sasa yanatumiwa na wanawake na wanaume.

“Nilianza kutumia mafuta ya BB wakati nilipokuwa katika jeshi kwa sababu pia yanazuia athari za jua kwa ngozi, na wakati ukiwa mwanajeshi wakati wote uko kwenye jua,” alisema Yu jin

“Nadhani wanaume wengi nchini Korea hujitunza hivi wakati wako kwenye jeshi.”

“Katika nchi za magharibi mwanaume akionekana akiingia katika duka la vipodozi, watu watashuku kuwa yeye ni shoga’’

Matamshi ya Jin yanaweza kuwaghadhabisha sana majenerali wa zamani , hata katika makaburi yao. Lakini kitu kimoja ni bayana, kuwa nyakati zinabadilika.

Kulingana na Lim Jung-shik anakadiria kuwa asilimia 20 ya wanaume nchini Korea Kusini wanatumia vpodozi, na hujipaka poda angalau zaidi ya mara moja. Na kwamba wengi hawaoni kama hili ni jambo baya.

“Hapa nchini Korea sio kama Marekani ambapo ikiwa watu watamuona mwanaume akiingia katika duka la manukato au vipodozi, watadhani kuwa ni mpenzi wa jinsia moja,” alisema Jin

“Miaka michache iliyopita kulikuwa na picha kwenye tangazo moja la biashara iliyokuwa na kauli mbiu kuwa unavyovalia ndio mkakati wako maishani, inakupa nafasi nzuiri katika nchi hii ambayo ina ushindani mkubwa katika sekta ya ajira”aliongeza Jin

Zaidi ya asilimia themanini ya wanafunzi hufuzu na kwenda katika vyo vikuu na ushindani wa kikazi ni mkubwa sana hapa.

Ikiwa hali ndio hiyo, anasema Yu Jin, kwa nini mtu asivalie vizuri kadri ya uwezo wake?

“Nadhani kwa wanaume sio etu tunataka kufanana na wanawake, lengo letu ni kufanana vizuri kama wanaume.

Je wanawake wanasemaje

Sio msanii huyu Psy wa 'Gangnam Style' pekee anayetaka kupendeza, ni kila mwanaume

“Yote haya ni kwa sababu wanaume wanataka kupendeza, nadhani ni jambo zuri,” alisema mwanamke mmoja

Hata hivyo hakupendezwa na wanaume waliojipaka rangi ya mdomo au Lipstick pamoja na wanja machoni.

“Jambo hilo halipendezi, lakini sipingi ikiwa kunao wanaofanya hivyo.”

Nini maoni yako kama mwanaume au mwanamke kuhusu wanaume kujipaka poda na vipodozi vingine?

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.