Nani ana ushawishi mkubwa Afrika?

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 11:56 GMT

Waafrika wanaodhaniwa kuwa na ushawishi

Kuna jambo moja ambalo limekosa jibu – ni kwa nini binadamu hawaishi kufuatilia maisha ya watu mashuhuri, matajiri na wenye vyeo vya juu maishani?

Kuna biashara nzima, na kubwa, inayoangazia maisha ya waigizaji mashuhuri na watu wengine mashuhuri – walichofungua kinywa nacho asubuhi, walichovaa, wanauhusiano na nani, na mambo mengine mengi yanayofaa kuwa ni maswala ya kibinafsi.

Kwa nini twafanya hivyo lakini? Ni kwa vile tungependa kuwa kama wao?

Au ni kwa sababu watu kama hao wanagusa maisha yetu kwa namna moja au nyingine?

Walipoulizwa, watu wengi walisema kwamba wangependa tu kuwa mashuhuri.

Jarida fulani limeorodhesha majina 100 ya Waafrika waliokuwa na ushawishi mkubwa mwaka 2012.

Baadhi ya waliopo ni majina ambayo yalitegemewa kuwepo – Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika Kusini; Aliko Dangote mfanybiashara mashuhuri wa Nigeria; Wole Soyinka, mwandishi kutoka Nigeria, mwimbaji wa Senegal Youssou Ndour na mchezakandanda Didier Drogba wa Ivory Coast.

Lakini ni kweli kwamba watu fulani wanaofikiriwa kuwa mashuhuri wana ushawishi wowote katika maisha ya raia wa kawaida?

Je ni ushawishi upi huu unaozungumziwa? Watu kama Didier Drogba au Youssou Ndour, ingawa ni magwiji kwa fani zao, wana ushawishi mkubwa katika maisha ya Waafrika kweli?

Ndio kuna baadhi ya watu kwenye orodha hiyo ambao,wanaweza kuwa na ushawishi lakini kuna tashwishi ikiwa ni wote waliotajwa.

wanachofahamu watu wengi ni kuwa ushawishi una maanisha uwezo wa kuhakikisha mambo yanafanyika kupitia shinikizo fuilani.

Mifuko ya misaada.

Mhisani mkubwa wa bara la Afrika Bill Gates

Cha mno zaidi ni vitendo kama hivi, vinaweza tu kukuathiri ikiwa utakuwa katika nchi fulani au sehemu fulani ya kazi.

Ndio, ni kweli kwamba viongozi wa nchi zilizoendelea kama Marekani na baadhi ya nchi za Bara Ulaya wana ushawishi fulani kwetu Waafrika kupitia mifuko yao mikubwa yenye fedha tele, na misaada wanayotupatia.

Kwa mfano, ni juzijuzi tu ambapo Uingereza ilisitisha msaada kwa Rwanda kwa ajili ya tetesi kuhusu jukumu lake huko Jamuhuri ya Kidemokrasa ya Congo.

Katika nchi jirani ya Uganda wahisani wa kimataifa walisema kuwa wataakhirisha mipango yao ya misaada kufuatia kashfa za ufisadi katika ofisi ya waziri mkuu.

Siki chache zilizopita, gavana wa benki kuu ya Uganda, alisema ikiwa wahisani wangetekeleza vitisho vya kuondoa ufadhili, nchi hiyo ingepunguza kasi ya ukuwaji.

Hatua zao bila shaka zingeathiri mamilioni ya watu nchini humo.

Mfano Didier Drogba,gwiji wa soka au Youssou Ndou mwanamuziki mashuhuri wa Senegal, wanaweza kusemekana kuwa na ushawishi.

Wamefanya mambo makubwa ambayo yamewasaidia kuafikia ndoto zao.Ndio wamegusa maisha yetu kwa njia moja au nyingine, lakini kuwa na ushiwishi kwa maana sawa ya ushawishi? baadhi wanahoji hili.

Mmoja wa watu anayeweza kusemekana amevuka mpaka na kuingia katika kitengo cha watu wenyeushawishi mkubwa duniani ni Bill Gates,aliyeanzisha wakfu wa kibinafsi wa kuimarisha afya duniani na kupunguza viwango vya umaskini.

Kitendo chake kimewagusa mamilioni ya watu maskini Afrika.

Nani unadhani ametosha kuwa na ushawishi Afrika?

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.