Kaunti ya Nairobi tarehe 16/12/12

Imebadilishwa: 16 Disemba, 2012 - Saa 15:20 GMT

Wanajopo Moses Ombati na Askofu Margaret Wanjiru.

Kipindi cha tatu cha Sema Kenya mjini Nairobi, kilizua mjadala mkali wakazi wakitaka majibu kuhusu usajili wa wapiga kura, uukosefu wa maji, ukosefu wa usalama na mengineo.

Kuwepo kwa watu mashuhuri katika jopo la Sema Kenya bila shaka kulichangia kusisimua mjadala kwani wagombea ugavana wawili; mwanabiashara Jimnah Mbaru na mbunge wa Starehe Askofu Margaret Wanjiru waliweza kushiriki.

Pia, Afisa Mkuu wa Polisi wa Nairobi Moses Ombati, mkuu wa Uchaguzi na Usajili wa Wapiga Kura nchini, Immaculate Kassait, Naibu wa Meya wa Jiji la Nairobi William Kinyanyi na mwanaharakati Joseph Kiarie (KJ) walijumuika na mjadala huyo.

Suala la usajili wa wapiga kura liliibuka wakazi wakiomba kuongezewa muda wa kujisajili. Ilibainika kwamba wengi kati ya wale ambao walikuwa hawajajiandikisha kupiga kura wangependa kupigia kura mashambani walikotoka. Hivi, waliomba muda wa kujisajili urefushwe hadi Disemba ili wakisafiri kuenda likizoni, wapate nafasi ya kujisajili.

Suala la usalama pia lilijitokeza, wakazi wakisema kuwa bado wanahofia kutokea kwa vurugu na rabsha baada ya uchaguzi.

Suala la ukosefu wa maji pia lilizungumziwa, baadhi ya viongozi wakiahidi kulitatua pale watakapochaguliwa na kuingia uongozini.

Kipindi hiki kilionyeshwa kupitia runinga ya KTN tarehe 16 Disemba 2012 na pia kupeperushwa hewani kupitia redio ya Idhaa ya Dunia ya BBC na vituo shirika; Pamoja FM, Star FM na KU FM.

Unaweza kukitazama kipindi hiki tena kwenye tovuti yetu hapa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.