Afrika Kusini 0 Cape Verde 0

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 17:45 GMT

Sherehe za ufunguzi za fainali ya mataifa ya Afrika

Mechi ya kwanza ya fainali za kuwania kombe la mataifa ya Afrika, moja ya mashindano makubwa zaidi ya soka duniani imekamilika nchini Afrika Kusini.

Wenyeji wa mashindano hayo, Afrika Kusini wamecheza na Cape Verde, ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Cape Verde ambayo ni taifa dogo zaidi duniani, ilifuzu kwa fainali hizo baada ya kuiondoa miamba ya soka barani Afrika Cameroon.

Katika mechi hiyo ya Ufunguzi, vijana hao wa Cape Verde wameonyesha mchezo mzuri na baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana nguvu ya kutofungana bao lote.

Hata hivyo katika kipindi cha pili wenyeji walizidi kuelemewa na Cape Verde ambao walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Kundi moja la kitamaduni wakati wa sherehe za ufunguzi

Wakati wa sherehe za ufunguzi, kulifanyika tamasha ya aina yake ambapo utamaduni wa nchi hiyo ulionyeshwa, kwa densi na musiki.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.