Angola 0 Morocco 0

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 21:18 GMT

Kikosi cha Angola

Angola imetoka sare ya kutofungana bao lolote na Morocco katika mechi ya pili ya michuano ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika, iliyoanza nchini Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya pili ya kundi A ilichezwa katika uwanja wa Soccer City,mjini Durban na Angola walipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Juhudi za mshambulizi matata wa Angola wa timu ya Real Valladolid, Manucho za kupachika magoli, hazikuzaa matunda, licha ya vijana hao wa Angolaa kuthibiti mpira wa asilimia kubwa.

Kocha wa Angola, Gustavo Ferrin amesema timu hiyo ipo katika mashindano hayo kwa malengo na amesema kuwa amefurahia matokeo ya mechi hiyo.

Naye kocha wa Morocco, Rachid Taoussi, kwa upande wake amesema hamasa ya timu yake ni kufika hatua ya mbele zaidi ya mashindano hayo.

Kufuatia matokeo hayo timu zote katika kundi A zina alama moja kila mmoja baada ya mechi ya ufunguzi katika ya wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde kumalizika kwa timu hizo pia kutoka sare ya tasa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.