Afrika Kusini kucheza Cape Verde

Imebadilishwa: 19 Januari, 2013 - Saa 13:43 GMT

Timu ya Bafana Bafana

Michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika inaanza leo, na Afrika Kusini inapepetana na Cape Verde ambayo inashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Jumla ya mataifa kumi na sita yanashiriki katika fainali hizo na kumi kati yao, yamewahi kutwaa ubingwa wa kombe hilo.

Ivory Coast, itakuwa ikishiriki katika fainali hizo kwa mara ya tano mfululizo kama timu inayopigiwa upato kutwaa ubingwa.

Ivory coast ilishinda na Zambia katika fainali iliyopita kupitia mikwaju ya penalti na Zambia na chini ya naodha wake anayecheza nchini Uchina, The Elephants, kama wanavyojulikana watajaribu kufuta machozi yao kwa kushinda kombe hilo.

Kwa mara nyingine tena dunia nzima itakuywa ikimtizama naodha wa timu hiyo Didier Drogba, ambaye ndiye ,mchezaji wa hadhi ya juu zaidi barani Afrika, licha ya kuwa alipoteza mkwaju wa penalti ambao uliiwezesha Zambia kushinda fainali.

Drogba kucheza mara ya mwisho

Didier Drogba

Fainali za mwaka huu vile vile ndizo zitakazokuwa za mwisho kwa Drogba ambaye ana umri wa miaka 34.

Hata hivyo Ghana amabyo ina wachezaji mahiri inatarajiwa kuwa mojawapo ya timu ambazo zinatarajiwa kutoa ushindani mkali kwa Ivory Coast.

Mabingwa watetezi, Zambia ambao wamerejea na kikosi kilichoshinda kombe hilo pia wanatarajiwa kufanya vyema.

Kutokana na umauzi wa Shirikisho la mchezo wa Soka barani Afrika, kuandaa mashindano hayo mwaka mmoja mapema, Zambia, itaandikisha historia ya kuwa timu iliyoshikilia kombe hilo kwa muda mfupi zaidi.

CAF, iliamua kuandaa mashindano hayo mwaka huu, ili kutogongana na michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia na vile vile kuruhusu wachezaji wanaoshiriki katika ligi mbali mbali dunia fursa ya kuakilisha mataifa yao.

Chipolo polo hata hivyo wamekuwa na matayarisho duni na kocha Herve Renard amesema kikosi chake ni bora kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita.

Timu ya Cape Verde

Renard ameimarisha kikosi hicho kwa kuongeza wachezaji wawili mshambulizi Jacob Mulenga anayeichezea klabu ya FC Utrecht striker na Emmanuel Mbola anayeichezea klabu ya FC Porto.

Ghana, nayo haijashinda kombe hilo kwa miaka 30 iliyopita lakini kutokana na kuwepo kwa wachezaji wengi wanaoshiriki katika ligi za ulaya, inatarajiwa kuandikisha matokeo mema.
Hata hivyo Ghana itakosa huduma za Andre Ayew, wa Marseille, Kevin-Prince Boateng, Sulley Muntari na Michael Essien.

Kocha wa Ghana Kwesi Appiah anamatumaini kuwa kikosi chake kinachojumuisha vijana chipukizi wakiongozwa na naodha wao Asamoah Gyan kitafanya vyema.

Mechi za Ufunguzi.

Kundi A: South Africa v Cape Verde, Angola v Morocco (siku ya Jamamosi)
Kundi B: Ghana v DR Congo, Mali v Niger (Jumapili)
Kundi C: Zambia v Ethiopia, Nigeria v Burkina Faso (Jumatatu)
Kundi D: Ivory Coast v Togo, Tunisia v Algeria (Jumanne)

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.