Awafunza waganda kunywa Kahawa

Imebadilishwa: 28 Januari, 2013 - Saa 12:46 GMT

Roberts Mbabazi

Bingwa wa biashara ya kahawa Afrika , (African barista champion) Roberts Mbabazi anaelezea changamoto ya kuwashawishi watu Barani Afrika ambako kahawa iligunduliwa, kuweza kunywa kahawa.

Ingawa athari za kahawai, zinasemekana kugunduliwa Afrika, kulingana na hekaya za zamani, na raia wa Ethiopia , watu hawanywi sana kahawa barani Afrika kama ilivyo kwingineko duniani.

Hilo limekuwa tatizo kubwa kwa mtaalamau na bingwa wa kahawa Roberts Mbabazi kutoka Uganda, nchi ya wanywaji wengi wa chai, na ambayo pia ni mzalishaji mkubwa wa kahawa aina ya Robusta duniani.

"Waganda hawanywi sana kahawa. Hiyo ndio imekuwa changamyo yangu kubwa. Mtu anaweza kukuuliza, ‘kwa nini kahawa? Kwa nini nisinywe chai? Kwa nini nisinywe soda au hata maji ya chupa?

Lakini anatumai kuwa hilo litabadilika huku idadi ya wananchi wa kiopatao cha kadri wakiendelea kuongezeka Uganda, kulingana na takwimu za benki ya maendeleo Afrika. Watu hao tayari ni asilimai 20 ya idadi ya wananchi wote Uganda.

Mbabazi angali anawafunza waganda kufurahia kikombe cha kahawa

"kuna wasafiri, watu wanaorejea nyumbani kutoka Marekani na Uingereza, na wanaelewa ambavyo kahawa inaburudhisha, wanaona utamaduni huo hapa na ninaamini kuwa ikiwa nitaendelea na kazi yangu hii hatimaye tutaweza kuondoa dhana ya watu kuhusu kahawa,’’ alisema Mbabazi.

Sasa ni hasa kazi ya mtaalamu wa kahawa? Anafanya vipi biashara yake?

"Ikiwa una tatizo lolote kuhusu kahawa , mimi nitakutatulia,’’ alisema Mbabazi.

''Ukitaka kufungua duka la kuuza kahawa niite tu, nitakuja kukusaidia . Nitakufafanulia kila mawazo yako na nitaweza kuyatekeleza. Ukitaka kufungua kampuni ya kukausha kahawa, nitakushauri kuhusu wateja wako kote nchini, aina ya kahawa wanayotaka.

Ikiwa wewe ni kijana anayetaka kupata ujuzi , nitakufunza ili uweze kupata kazi maishani mwako.''

Ikiwa wewe ni mkulima na unataka kuboresha zao lako , unataka kuwa na mazao mazuri , basi niite tu na nitaweza kukushauri utakavyoweza kununua kahawa , utakavyoikausha na namna ya kuiandaa kwa mauzo.’’ Alisema Mbabazi.

Mjasiri amali huyu mwenye umri wa miaka 24 aliongeza kuwa pia anaweza kutoa ushauri wa kitaalamu kwa viwanda vya kahawa kuhusu uboora wa kahawa yao.

Ufanisi wa kutengeza kahawa

Bwana Mbabazi alianza kampuni yake Barista Pro Coffee, mwaka 2010.

'Barista' ni mtu ambaye ana taaluma ya kutengeza na kupakua kahawa katika mkahawa wa kahawa.

Lakini kwa watu wa sekta hiyo, pia inamaanisha taaluma ya hali ya juu. Wataalamu wazuri wa kahawa wanapaswa kujua kwa undani mbinu ya kutengeza kahawa kwa ukamilifu kutoka kwa upanzi na kuvuna pamoja na kuiandaa kwa kuikausha pamoja kuitengeza kama kinywaji.

Mbabazi alianza kujhusisha sana na kahawa pindi alipomaliza masomo yake ya shule ya upili upili mwaka 2004.

Alitoka katika familia maskini na aligundua kuwa hangeweza kupata karo ya chuo kikuu na hivyo kulazimika kutafuta ajira.

Mwanzo alifanya kazi kama muuza duka , lakini mshahara ulikuwa mdogo sana, na kisha akaanza kutafuta kazi nyingine na hivyo akatafuta kazi katika mikahawa , vilabuni na hata kwenye bar.

  • Umri: 26, mzaliwa wa Magharibi mwa Uganda.
  • Alimaliza shule mwaka 2004 na kufanya kibarua katika mikahawa, bar na vilabu
  • Alianza kampuni yake ya Barista Pro Coffee, mwaka 2010. Anawaajiri watu wanne

Katika moja ya bar hizo, mjini Kampala, ndiko alijifunzia kutengeza kahawa.

Na hapo ndipo pia alifahamu kuwa Uganda kama nchi ambayo inapanda kahawa, haina wanywaji wengi wa kahawa.

Mwaka 2006, alianza kazi katika mkahawa wa shule moja ya densi mjini Kampala, mwaka uliofuata na kujiunga na taasisi ya mafunzo ya kutengeza kahawa yaliyoandaliwa na halmashauri ya kahawa ya Uganda.

Baadaye alishinda mashindano ya mtengezaji bora wa kahawa mara tatu na kuwakilisha nchi yake ambapo aliweza kupokea mafunzo nchini Canada na Uholanzi.

Mwaka 2012 alishiriki mashindano nchini Ethiopia na kuwa bingwa wa kutengeza kahawa.

Mapato mazuri

Bwana Mbabazi aliambia BBC kuwa alitumia dola elfu saba kuanzisha kampuni yake. Sehemu kubwa ya pesa hizo, alizitumia kununua machine za kutengeza kahawa ya espresso na vifaa vingine.

"Kabla ya hapo, nilihitaji muda mwingi zaidi. Nililazimika kukaa nje sana na muda mwingi sikuwa na familia yangu. Nilisafiri sana kati ya Marekani na Canada na hata nchini Switzerland, kujifunza mambo mengi kuhusu kahawa.’’ Alisema Mbabazi.

Mbabazi anapenda kuzungumza na wakulima wa kahawa akiwashauri namna ya kupata mazazo mazuri

Mtaji wake ulikuwa pesa alizokuwa ameweka akiba kutokana na mishara ya kazi zake za kwanza.

Mshahara wake sasa ni karibu dola elfu moja miambili, na anasema kwa kijana kama yeye mshahara huu unamtosheleza.

Anawaajiri wafanyakazi wengine wanne. Angependa kurejea shuleni katika siku za usoni lakini kwa sasa anaonelea bora kutumia pesa alizonazo kwa kahawa. Pia anapenda kuwafunza watu,

"Naamini naweza kutimiza ndoto yangu ya kurejea shuleni siku moja, lakini kwa sasa napenda kazi yangu ya kahawa,'' alisema Mbabazi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.